Tunahitaji kujua kwa sababu hatujui; na hatuwezi kujua kama hatujui kwamba hatujui...Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi. Na kadiri tunavyojua, ndivyo tunavyogundua kwamba hatujui...
Tuesday, January 29, 2008
Kofi Anna bado amekwama Kenya
Ufumbuzi wa mgogoro Kenya bado ni mgumu. Mauaji yanaendelea, huku Mwai Kibaki na Raila Odinga hawajakubaliana mahali pa kuanzia mazungumzo, bado wanashitakiana kwa mauaji ya kimbari. Na kwa mara ya kwanza, mwansiasa, mbunge wa upinzani kauawa na kuibua ghasia mpya. Wakati huo huo, jamii inaendela kumshinikiza Kibaki ajitoe mhanga kuleta amani. Sasa Kofi Annan na timu yake ya wapatanishi wametoa ajenda ya mjadala wa usuluhishi. Itakubalika sawa kwa pande zote?
Friday, January 25, 2008
Tuesday, January 22, 2008
Raila ampeleka Kibaki kizimbani
Ukisikia Nguvu ya Umma ndiyo hii. Matukio haya yanaendelea kudhihirisha kwamba sasa Kenya inaongozwa na marais wawili. Mmoja wa kuchaguliwa na wananchi na mwingine wa kupachikwa na Tume ya Uchaguzi. Mmoja anashikilia na kutumia vyombo vya dola, mwingine anashikilia na kutumia imani ya wananchi. Acha Kibaki akae Ikulu, lakini kama analala usingizi, basi si binadamu mwenzetu. Moto bado unawaka, na kama mambo yataendelea hivi, na hasa baada ya ODM kumfikisha kizimbani, cha moto atazidi kukiona. Soma mwenyewe.Wakati huo huo, mambo yanaanza kupata mwelekeo nchini Kenya baada ya Kofi Anna kuanza kazi ya usuluhishi na upatanishi. Baadhi ya mapya mpya haya hapa. 0. 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10.
Sunday, January 20, 2008
CCM ya ufisadi na utumwa
Msanii huyu wamemnunua, wakampa ajira na uanachama, na wakamuahidi makubwa, halafu wakamnyima. Sasa ameamua kubwaga manyanga na kuwarudishia kadi yao. Nionavyo mimi, kununua na kuchuuza binadamu wenzetu ni ufisadi na ni utumwa unaoendekezwa na CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuph Makamba. Soma na toa maoni yako.
Friday, January 11, 2008
Hongera Dk. Slaa

Kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfukuza kazi Gavana wa Benki, Daudi Ballali, ni jambo la kutia moyo. Pongezi anazopata Rais Kikwete sasa anazistahili. Lakini sote tunajua kwamba Rais Kikwete amelazimika kuchukua hatua hizo, ingawa serikali ilikuwa inajua 'matatizo' ya Benki Kuu. Kama si Dk. Willibord Slaa (pichani) na wenzake kuibua hoja hiyo Bungeni na kushinikiza serikali ichukue hatua, uchunguzi usingefanyika, na hatua hii moja isingechukuliwa. Kwa sababu hiyo, wanaompongeza Rais Kikwete wasimsahau yule aliyemsukuma, Dk. Slaa.
Haya yote yameonyesha kuwa serikali na watu wake ilijua ukweli wa tuhuma alizotoa Dk. Slaa, ndiyo maana hata Jaji Mark Bomani akawaonya waliotishia kumshitaki mtoa tuhuma, ambao waliishia kutoa vitisho lakini hadi leo hawajakanyaga mahakamani. Na sasa tayari ametangaza kuwa ana siri nyingine kubwa za wizi wa vigogo. Ndiyo maana nasema, katika hili la JK kuchukua hatua, shujaa ni Dk. Slaa. Na tayari kuna dalili kwamba Ballali hatakubali kutolewa kafara na kufa peke yake.
Tetesi zinazovuma sasa, kutokana na usiri wa serikali juu ya suala la Ballali, ni kwamba ugonjwa wake ulisababishwa na sumu aliyolishwa kumkolimba, ili siri zao zisitobolewe! Lakini sasa inasemekana naye kaamua kufa na serikali.
Tuesday, January 08, 2008
Asanteni
Kwa unyenyekevu mkubwa, nawashukuru walionipendeza kwa tuzo hii ya Excellence in ICT Journalism katika Afrika. Siwajui, wanajijua. Nawashukuru na majaji walionipigia kura. Asanteni!
Sunday, January 06, 2008
Wahariri wakatwa mapanga
Wapambanaji wenzetu wawili, Ndimara Tegambwage na Saed Kubenea, wanaochapisha gazeti la MwanaHalisi wamevamiwa ofisini na kukatwa mapanga Jumamosi 6, 2008 katika ofisi za gazeti hilo, Kinondoni, Dar es Salaam. Tayari hisia za wananchi zinawatuhumu baadhi ya mafisadi serikalini na wapambe wao, kwa kuandaa 'ujambazi huu.'
Kubenea ndiye Mhariri Mtendaji na mmiliki wa gazeti hilo, wakati Ndimara ni Mhariri Mshauri na 'mashine' ya kitaaluma ya gazeti hilo.
Gazeti hilo limekuwa na makala na habari kali mno dhidi ya wezi ndani ya serikali. Mara kadhaa Kubenea ameonywa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa barua, simu na mdomo. Kuna wakati gazeti 'lilivamiwa' na watendaji wa serikali kwa kisingizio cha kukagua 'uwezo wa kitaaluma wa waandishi' wa gazeti hilo. Mara nyingine lilivamiwa na watu wa TRA, eti kutazama kama linaipa kodi.
Vile vile, ndilo hazeti lililowahi kumtuhumu kiongozi mmoja wa juu serikalini, ambaye lilimuita Bwana 'mvi' kwa kuwaagiza wahariri kadhaa rafiki zake waanze mkakati wa kuwaandama wakosoaji wa serikali.
Ikumbukwe kwamba ndilo gazeti pekee lililotaja majina ya mafisadi waliotajwa na Dk. Willibroad Slaa bila kificho, mbele ya umma, pale Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

Tujadiliane

Mwaka 1991, aliyekuwa Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda alishindwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu, akawakabidhi madaraka bila ghasia. Mwaka 2000, aliyekuwa Rais wa Senegal Abdou Diouf alikabidhi madaraka kwa washindi na kuondoka Ikulu kwa amani. Mwaka 2002, aliyekuwa Rais wa Kenya, Daniel arap Moi, alimkabidhi Mwai Kibaki (pichani kushoto) uongozi, baada ya mteule wake aliyeandaliwa kuwa mrithi wake, Uhuru Kenyatta wa KANU, kushindwa na nguvu ya upinzani.
Mwai Kibaki aliyepishwa na Moi, ameshindwa kukubali matokeo baada ya miaka mitano tu ya kukaa Ikulu na kukataliwa na wapiga kura. Ghasia zimezuka, damu zimemwagika. Amejiunga na klabu ya marais wezi wa kura, kina Robert Mugabe na Amani Karume. Tanzania tunajifunza nini? Afrika yetu inaelekea wapi? Tufanye nini kuinusuru? Hawa wametoa maoni yao. Wewe una maoni gani? Tujadiliane.
Friday, December 28, 2007
Matokeo ya Uchaguzi Kenya
Fuatilia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2007 hapa. Inaeleka wenzetu wameamua kufanya 'mapinduzi ya awali ya uongozi.' Hadi sasa Raila Odinga wa ODM anaongoza; Mwai Kibaki wa PNU anafuata nyuma. Kalonzo Musyoka wa ODM-Kenya yuko mbali sana. Muujiza alioutarajia haujatokea! Umebaki kanisani! KANU kimeanza kupotea katika historia ya utawala wa Kenya. Endelea. Linganisha na hii pia.
Monday, December 24, 2007
Krismasi Njema

Napenda kuwatakia Krismasi Njema! Krismasi ni tukio lenye maana mbalimbali kwa watu mbalimbali. Kwa wengine ni 'kumbukumbu' ya kiroho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2007 iliyopita. Kwa wengine ni tukio kubwa lililoigawa historia katika ngwe mbili - Kabla ya Kristo na Baada ya Kristo. Kwa wengine (hasa Ulaya Magharibi) ni wakati wa kumaliza mwaka, kujipongeza na kujiandaa kwa mwaka mwingine; ni kipindi cha manunuzi na matanuzi. Kwa wengine halina maana kabisa, lakini wanajikuta wakiungana na wenzao wanaosherehekea Krismasi. Kwa wote hao, nasema Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2008.
Wednesday, December 19, 2007
CHADEMA na CCM: nani mwizi wa sera?
Vyama vya siasa vinaposhutumiana kwa kuibiana sera maana yake nini? Je, kati ya CHADEMA na CCM, ni kipi kimedhihirika 'kuiba' sera za mwenzake? Kuna mifano hai? Inaaminika? Tutafakari.
Sunday, November 25, 2007
Tusiogope, Mapinduzi Yanawezekana

Nina hoja mbili. Kwanza, tuwe na rais wa kukaa mdarakani miaka mitano badala ya miaka kumi. Pili, tukubali kwamba maendeleo tunayotaka kuyafanya hayawezekani kama hatutakubali kuanza sasa kufanya mapinduzi. Wengine wana shaka, na wengine wanadhani haiwezekani. Lakini kama iliwezekana kwa Warumi, (mtazame Kaizari Julius pichani na utafakari yaliyomkuta) itashindikanaje kwa Watanzania? Na je, kushuka kwa umaarufu wa Kikwete kwaweza kuwa ishara mojawapo ya mwanzo mpya? Au ndiyo wanaanza kujifunza Afrika Kusini na Kenya, kujitambua na kugundua makosa?Tujadiliane.
Wednesday, November 07, 2007
Kuna ukweli gani katika hili?
Ujumbe huu unazunguka katika barua pepe za watu. Ulipofika kwangu nikaamua niuweke hapa tuujadili wazi wazi. Unasema hivi:
"Je tutafika? ...tuhuma zote za ufisadi zinazoikabili BoT, je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa. Ndani ya mtungi wa BoT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BoT ni pamoja na hawa wafuatao:-
1. Pamella Lowassa,
2. Filbert Frederick Sumaye,
3. Zalia Kawawa,
4. Harieth Lumbanga,
5. Salama Ally Mwinyi,
6. Rachael Muganda,
7. Sylvia Omari Mahita,
8. Justina James Mungai,
9. Kenneth John Nchimbi,
10. Blassia Blassius William Mkapa,
11. Violeth Phillemon Luhanjo,
12. Liku Irene Katte Kamba,
13. Thomas Mongella,
14. Jabir Abdallah Kigoda etc.
Hapa nani atamwajibisha Dalali alas Balali? Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO? Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na wazito wa nchi, wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya (mere coincidence). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika."

Tuesday, November 06, 2007
Mkaribisheni Peter Nyanje
Mkaribisheni Peter Nyanje, mhariri wa habari wa gazeti la Tanzania Daima katika ulimwengu wa blogu. Ameingia na kuahidi makubwa; na anatualika "tujadili hoja nzito." Tunaamini ataitumia blogu yake kuwaletea wasomaji kile wanachokikosa katika gazeti lake, yaani kile kilicho muhimu kinachobaki na kukosa nafasi katika habari za kawaida za kila siku. Blogu yake hii hapa. Mtembeleeni.
Kikwete mfa maji?

Usimshangae Rais Jakaya Kikwete. Huu ni mkakati wake. Wakati mawaziri wametoka mikoani majuzi kulaani kauli za wapinzani kwamba ni uzushi, yeye amesema wapinzani wasipuuzwe. Na baada ya kuona wananchi wanapuuza hoja za utetezi wa CCM na kukumbatia za wakosoaji kuhusu masuala ya madini, sasa rais anataka kuunda kamati ya madini itakayowashirikisha hata wakosoaji wake hao hao. Je, anataka kuwaziba mdomo wanaoikosoa serikali? Na tayari ameahidi kuwapa hela ya kutosha na ziara nje ya nchi kwa kazi hiyo. Ni hongo? Anataka kumaliza nguvu za upinzani kiujanja ujajanja? Au ndiko kutapatapa kwa mfa maji?
Sunday, October 28, 2007
Taarifa hizi zinatisha
Sasa tumeanza kuelewa kwa nini serikali inajikanyaga kuhusu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa na wapinzani. Taarifa mpya mpya zinaonyesha jinsi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilivyotumika kuibia pesa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 ili mgombea urais wa CCM ashinde kwa kishindo. Binafsi naamini kwamba, kwa mazingira yaliyokuwapo, mgombea wa CCM angeshinda hata bila ya kununua kura. Soma mjadala hapa.
Friday, October 26, 2007
Habari Corporation yafungua tovuti

Kampuni ya Habari Corporation, inayomilikiwa na Mbunge wa Igunga na Mhazini wa CCM, Rostam Azizi (pichani kushoto), imefungua tovuti ya magazeti yake. Magazeti hayo yaliyowahi kutamba kwa uchambuzi mahiri na makini katika miaka ya 90 na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, yanapatikana hapa. Siku hizi inaitwa New Habari Corporation - yenye mmiliki mpya, sera mpya mikakati mipya na uongozi mpya.
Friday, October 19, 2007
Satan's benefit in our deeds
A man woke up early in order to have his morning
devotion (prayer) in the Lord’s house (church). He
got dressed, set on his way to the Lord’s house (church).
On his way to the church, the man fell and his clothes
got dirty. He got up, brushed himself off, and headed home.
At home, he changed his clothes, and was, again,
on his way to the Lord’s house. On his way to the
church, he fell again and at the same spot! He,
again, got up, brushed himself off and headed
home. At home he, once again, changed his
clothes and was on his way to the Lord’s house (church).
On his way to the house of God (church), he
met a man holding a lamp. He asked the man of
his identity and the man replied, "I saw you
fall twice on your way to the house of God (church),
so I brought a lamp so I can light your way.
The first man thanked him profusely and the two
were on their way to the house of God (church).
Once at the house of God (church), the first man
asked the man with the lamp to come in and
pray with him. The second man refused. The
first man asked him a couple more times and,
again, the answer was the same. The first man
asked him why he did not wish to come in and pray.
The man replied, "I am Satan". The man was shocked
at this reply. Satan went on to explain, "I saw you on
your way to the house of God (Church) and it was I
who made you fall. When you went home, cleaned
yourself and went back on your way to the house of God
(church), God forgave all of your sins. I made you fall
a second time, and even that did not encourage you to
stay home, but rather, you went back on your way to Church.
Because of that, God forgave all the sins of the people of
your household. I was afraid if I made you fall one more
time, then God will forgive the sins of the people of your village,
so I made sure that you reached the house of God (Church) safely.
" So do not let Satan benefit from his actions.
Do not put off the good you intended to do, as you never
know how much reward you might receive from the hardships
you encounter while trying to achieve that good. For your
righteousness can save your family and nation at large. Do
this and see the victory of the Lord.
Note: It was forwarded to me by a friend. I thought it might make a good reading for visitors of this blog. Stay blessed!

Sunday, October 14, 2007
Huyu ni Mwalimu wangu
Mama huyu ni mmoja wa walimu wangu. Anaitwa Prof. Susan Miller. Cheo chake ni MBA Academic Director, katika Chuo Kikuu cha Hull. Mpiga picha alinikamata nikiwa nasisitiza jambo - ona mikono, utadhani nasali vile! Teh! teh! teh! Picha hii ilipigwa Alhamisi wiki hii mara baada ya mlo wa jioni ulioandaliwa na Hull University Business School kwa ajili ya wanafunzi wote wa MBA chuoni hapo. Uwongo mbaya, kazi anaiweza.
Friday, October 12, 2007
Kikwete anasaidiwa na Ze Comedy?

Kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi (akiwamo yeye) haina 'mashiko.' Ukichanganya kauli yake, ya Kingunge Ngombale-Mwiru, na ya Jaji Joseph Warioba, utaona kwamba hapa kuna kutapatapa kwingi. Nashangaa magazeti yameandika JK ajibu mapigo. Nimesoma kwa makini, lakini sikuona hata pigo moja alilojibu. Hata waliosema ametoa majibu mazito wamemkweza bila sababu. Sikuyaona. Kama waliomtangulia kutoa kauli, analenga lakini ameshindwa kuwachanganya wananchi. Lakini kwa kuwa yeye alipewa muda mrefu kusoma alama za nyakati, na kwa kuwa yeye ndiye mkuu wao, wananchi walitarajia kauli pevu zaidi kutoka kwake. Haijapatikana.
Nadhani wapinzani wamemjibu vema. Ametonesha vidonda. Na bado yataibuka mengine tu. Rais ameibua maswali magumu. Nami bado ninaye; namtafakari. Katika hili, siko peke yangu. Tazama mchambuzi mwingine alivyomfanyizia Kikwete. Sasa nasikia wasanii wa Ze Comedy wameanza kuigiza tuhuma za vigogo, huku wakiwatetea watuhumiwa na kumsakama Dk. Slaa. Niko mbali na nyumbani. Wanaojua walete habari kamili. Inawezekana CCM imeamua kuwekeza katika Ze Comedy kuwapumbaza Watanzania, kuwatetea mafisadi?
Subscribe to:
Posts (Atom)
- Ansbert Ngurumo
- Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'