
Sielewi Jaji Joseph Sinde Warioba amekuwaje. Kiongozi mstaafu, mwanasheria mstaafu na mtu aliyewahi kuongoza tume ya rushwa anaposema 'tuhuma hizi si mpya,' anataka kusema alitarajia kuona mpya zipi? Au alitaka hizi za zamani ziachwe tu? Simwelewi. Namshangaa pia anapoona kwamba kujadili rushwa ya wakubwa si muhimu kwa maendeleo ya nchi. Zaidi nipale anapopata shida kuelewa kwanini rais na rais mstaafu wanatuhumiwa. Nadhani angepaswa kuwashangaa wao na kujiuliza: "kwanini watuhumiwe? Kwanini wao na si wengine?" Badala yake, anawatetea kana kwamba anatoa 'hukumu kuwasafisha.' Bado simwelewi. Hivi hajui kwamba Tanzania itakuwapo bila yeye wala Jakaya Kikwete au Benjamin Mkapa?