Saturday, September 08, 2007

Nimekutana na Ndesanjo

Tayari nimefika Grahamsatown, alasiri Jumamosi Septemba 9, 2007. Nimekutana na Ndesanjo Macha kwa mara ya kwanza, ana kwa ana. Muda wote tulikuwa tunafahamiana kupitia blogu na magazeti. Baadaye jioni tutakuwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Digital Citizen Indaba kama nilivyoeleza hapo chini.

2 comments:

Jeff Msangi said...

Hongereni wanablog wenzetu.Utakumbuka jinsi ilivyokuwa raha mimi na wewe tulipokutana ndani ya Toronto mwaka jana.Zile picha zenye tabasamu natumaini bado unazo.

Niliona swali uliloniuliza pale kwangu.Mimi bado nipo hapa hapa uliponiacha mwaka jana.Bado nakatiza mitaa ile ile,nikiwaza yale yale na mengi zaidi.Nikitizama taa za usiku,mbalamwezi na nyota nikitafakari lini nchi yetu nayo itafikia hapa au pale.Ninawatakia mkutano mwema.

Egidio Ndabagoye said...

Tunawatakia upeperushi mzuri wa bendera yetu.
Tunawafilia kinachojili huko

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'