Saturday, September 15, 2007

Pole Mheshimiwa Mudhihir


Mbunge wa Mchinga (CCM), Mudhihir Mohammed Mudhihir akipokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Ijumaa septemba 14. 2007, akitokea Lindi alikopata ajali ya gari. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Saidi Mecky Sadick. Picha kutoka Daily News.

Ajali haina kinga. Yaliyompata Mudhihir yanaweza kumpata mtu yeyote. Zaidi ya hayo yanawapa abiria wengi katika ajali za barabarani na angani kila siku. La msingi, tumshukuru Mungu kwamba Mudhihir yuko hai. Tumpe pole na kumwombea apone haraka.

4 comments:

Samuel said...

Pole mheshimiwa mbunge. Ya kawaida hayo,yamekuwa yanawapata wananchi wako kila mara kutokana na ubovu wa barabara au uendeshaji mbaya wa madereva. Heri wewe upo hai, wenzio walishatangulia! Pole.

Anonymous said...

Jamani sijui kama bunge lijalo atakuwa ndani ya nyumba. wakati wengine wanasimamishwa na wanadamu kutimiza matakwa ya wengine, wengine wanasimamishwa na muumba wao. anyway yote maisha.

Babu said...

Huo ulemavu unaweza kuwa kipandio cha ubunge, chama kikamwonea huruma na kumteua na wananchi wakapiga kura za huruma. Si unawajua wananchi wetu?

anonymous said...

mmoja anasema sawa!
hila issue ipo kwenye,

kufunga kamba za viatu!

kushika kopo la maji msalani ili kutawadha/kuchamba.

kukumbatia.

kuvaa condom

kuvuta sigara huku na glass ya beer mkononi!

kumkunja na kuchapa mtu makofi kama ilivyotokea kwa Asha Baraka.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'