Sunday, September 09, 2007

Kutoka Grahamstown

Jamaa alinikamata vizuri na kamera yake nilipokuwa nawasilisha mada yangu. Leo Septemba 10. 2007 imekuwa siku ya michakariko. mimi, Ndesanjo na Bob Sankofa tumekuwa tunawasilisha mihadhara yetu kwa wasikilizaji waliokuwa katika Digital Citizen Indaba. Tumejumuika na waandishi wengi kutoka sehemu mbalimbali za Afrika. Hotuba ya ufunguzi wa mjadala wa leo katika Indaba imetolewa na Ndesanjo. Pata sehemu ya mhadhara wa Macha hapa. Nitawaletea taarifa nyingine baadaye. Zoopy wameweka hapa sehemu ya kilichotokea.

1 comment:

Chuma said...

Nilidhani makali yako ni katika kuandika tu, kumbe hata haya unayaweza? Hongera mkuu! lakini, nisisahau..wewe si ulijifunzia kuhubiri? sawa hapa ndipo pake.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'