Wednesday, September 19, 2007

Kingunge ang'atuke


Pamoja na mambo mengine, natoa wito. Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru ang'atuke. Badala ya kushauri vijana wake wajiheshimu n akutimiza wajibu wao, anafanya kazi ya mganga wa jadi kwenye masuala mazito! Naona Mpayukaji tayari ameniunga mkono.

14 comments:

Selina said...

Babu kachoka, hata propaganda haziwezi tena.

kamala J Lutatinisibwa said...

huyu mzee aondoke akalime. yaani anafikiri vijana tunaweza kumwamini? yeye na akina nyerere wamekuwa wakipiga vita njaa, maradhi, ujinga na umaskini. lakini pamaka leo tumeongeza maadui hata rushwa, mikataba bomu etc. kwa nini askubali kushindwa? ccm inahitaji kizazi kipya. kingunge amepitwa na wakati tu, amechoka. yawezekana serikali ya kikwete inaboronga kwa sababu ya kuwa na akina kingunge wasiokuwa na jipya.

Kalundi said...

Babu inafaa akapumzike sasa, wenzie wakinaMkali wanajuta kutosoma alama za nyakati!! Yeye ndiye aliyempa Jakaya Urais kwa kumtetea madhambi yake yasianikwe mbele ya kamati kuu wakati wa mchakato sasa inafaa akale pension yake!! Lakini inaelekea hataki kung'atuka kwani bado angombea ujumbe wa NEC. Inafaa vijana wampige lungu la kichwa akose kuchaguliwa!!

Ansbert Ngurumo said...

Kalundi,

Usikose gazeti la Tanzania Daima Jumapili. Huyu Babu kaguswa kwenye Maswali Magumu.

Anonymous said...

Kwalipi baya analifanya? Ngurumo unachemsha...Kimsingi wakalie kidedea watu wenye FULL authority. yeye kawa mshauri wa CCM na serikali yake, Kama CCM haifai sema CCM na Serikali yake Haifai na sio unachagua wachache na kuwapaka rangi..CCM yote ing'atuke...

Ansbert Ngurumo said...

Bwana Anonymous,
Huoni baya katika kauli zake hii? Huoni usaliti wake kwa wananchi wanyonge, maskini, walalahoi wa Tanzania? Huoni athari za ufisadi huu kwa hatima ya maisha ya wananchi? Kwa umri huo, na kwa nafasi aliyonayo, huo ndio ushauri anaowapa? Huoni kwamba wanapotosha viongozi anaowashauri na wananchi anaopaswa kuwatumikia?

Yawezekana wewe na yeye mmeshiba au maona maslahi yenu yanaguswa. Lakini kumbukeni masalhi ya wengi kuliwa na wachache si haki itokayo kwa Mungu. Ni heri kukosa kiongozi asiye na upeo kuliko kuwa naye akawapotosha namna hii. Kama sababu ni umri au uwezo mdogo, au yoyote tusiyoijua sisi, inatosha kumfanya Kingunge ang'atuke. Yeye mwenyewe ameshiriki kung'atua wengine. Na amesema akasikia na kunukuliwa kwamba: "Asiyetaka kung'atuka atang'atuliwa." Yeye akiyasema kwa wengine sawa. Sisi tukiyasema kwake tunahojiwa
"kafanya baya gani?"

Anonymous said...

Mimi Naona kuwa kwa sababu ya uzee wake ndio amefanya hivyo.. maana yeye anajua kuwa yupo katika mfumo wa kimla hapa sasa hivi! Naona ingekuwa vizuri sana angeongea na watu wa CCM Chiwaga pale DOdoma . na kama ndio ushauri anaotoa kwa Rais ndio huu basi ni matatizo makubwa sana. Ni ni hatari kabisa kwa mzee kama huyu kusema hivyo. Achane kuona kama vile yeye ndio yeye huko tanzania.
John

Anonymous said...

hivi, kwa nini mola anaweka vizee kama hivi duniani. kwa nini asingeturudishia akina moringe na kukichukua kibabu hiki? hakifai kwa lolote. muafaka unakwama kwa sababu chenyewe kimeshikilia fikra za kizamani, enzi za mkoloni. hebu na kifilie mbali. na kikifa hatutaki kusikia eti hela zetu zimetumika kwa maziko yake ya kitaifa. familia yake watumie fedha alizotuibia na kutupora kuendesha mazishi yake. tena nataman yawe kesho.

Darweshi said...

Taratibu, Mola anaanza kusikiliza sala zea wanyonge. soma hapa uone jinsi mabalaa yanavyoanza kuwakuta watu wa CCM waliomfanyia Zitto mtima nyongo.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=75383#post75383

jingo said...

huyu mzee,angekuwa na busara angejiuzulu nafasi nyeti aliyonayo katika serikali na kubaki na ujumbe katika chama chake cha ccm,lakini anakoelekea na uking'ang'anizi na uchu wa madaraka hatajifunjia heshima na recodi tete aliyojijengea kama mkomunist,
hivi sasa amejivika uwakili kuwatetea MAFISADI 11 waliotangazwa na Dr.Slaa na mwanaharakati Tundu Lissu unategemea nini hapo?
punde tu atakula matapishi yake ya "usipong'atuka utang'atuliwa."

nawasilisha!

Anonymous said...

ndugu zangu, nadhani raha ya mjadala ni kujenga hoja kwa jambo la msingi. Kunishambulia kwa matusi na kashfa, ni jambo jema, na kwa muungwana yeyote, kwenye akili inayokata kama wembe, hawezi kutumia lugha ya kashfa. Kusema kichwani kwa manyerere hakuna kitu, na kwamba kaambulia safari ya cuba pekee, ni uwongo na kupotosha mjadala.

Siriha said...

Hatupotoshi mjadala "kamanda" huu ni ukweli ulikuwa kwenye delegation ya mtawala wetu Cuba hata ukatupigia picha ya mwanamtandao mwenzio Rweikiza Mukandala akiwa na Mtawala wetu Cuba. Picha hiyo uliitoa alipozawadiwa uvicechancellor wa mlimani kwa kazi aliyoifanya kumpamba JK wakati wa mchakato kwa kutumia REDET. Unabisha?

Anonymous said...

Huyu mzee anatetea mambo yake ya kituo ch mabasi Ubungo yasitajwe!! Nani asiyejua pafukapo moshi kuna moto? Lazima kuzima haraka japo wameshachelewa

Anonymous said...

Very nicce!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'