Monday, September 10, 2007

Hii nayo kali

Zamani Shirika letu la Ndege (Air Tanzania Corporation), kwa sababu ya kutokuwa na huduma inayoaminika, liitaniwa na wabongo, likaitwa Any Time Cancellation (ATC). Wanigeria nao sasa wameibuka na mpya kuhusu 'TANESCO' yao. Kwa sababu ya mgawo wa umeme na matatizo yasiyoisha, mamlaka yao ya umeme iitwayo Nigerian Electric Power Authority (NEPA), imekuwa ikitaniwa na kuitwa Never Expect Power Always (NEPA).

Ili kukabiliana na tatizo la umeme, serikali imeifanyia mabadiliko ya kimfumo, kiutawala na kiuendeshaji, ikaundwa kampuni iitwayo
Power Holding Company of Nigeria (PHCN). Matatizo ya mgawo yamebaki pale pale, na sasa wanaiita Problem Has Changed Name (PHCN).

4 comments:

Anonymous said...

Sooo funny!!
Kila la kheri ngurumo endelea kutuelimisha. Inaonekana huko kwa wenzetu blogging ni kitu muhimu sana. Tunasubiri uchambuzi wako and the way foward kabla ya mkutano wa Nairobi

Ansbert Ngurumo said...

Analyst, asante. Nitajitahidi kutimiza wajibu wangu.

projestus rwegarulila said...

ebwanae,
Nimefrahishwa sana na jinsi ulivyo kokotoa rushwa ndani ya chama tawala.Na hata ukanifungua macho zaidi kuhusu jinsi ilivyo rahisi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko kitengo cha rushwa kutokuwa chini ya ofisi ya rahisi.
Vile vile napenda uwe mhamasishaji uzalendo wa nchi yetu.mimi naishi ughaibuni hapa lakini sifrahishwi na mambo yanavyokwenda katika utawala mzima huko nyumbani.Natamani Nyerere angefufuka akawakuta hawa walarushwa ambao hawana hata mtu wa kuwakemea. mfurukutwa toka bk

Pen Ultimate said...

Air Tanzania = Air Labda, sivyo?

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'