Monday, September 10, 2007

Wameandika hivi juu yetu


Tukiwa Grahamstown, tulitumia vema fursa tuliyopata kuzungumza na Waafrika wenzetu katika midahalo,. mijadala na kongamano. Mara ya kwanza ilikuwa katika Digital Citizen Indaba, Jumapili asubuhi, ambapo mimi, Ndesanjo na mwandishi wa Kenya Daudi Were tulijadili mada ya fractured identities. Mimi nilizama katika kueleza umuhimu wa kublogu wa Kiswahili. Baadaye Mpiga Bob Sankofa alitoa mhadhara kwa nini anablogu kwa kutumia picha. Tumetoa ujumbe. Umefika. Baadhi ya waandishi waliokuwapo wameandika hivi juu yetu. Mwingine huyu hapa. Pia usikose stori hii. Kumbe hata wapiga picha hupendeza wakipigwa picha. Muone BOB SANKOFA akihojiwa na mapaparazi kama yeye. Pichani, kutoka kushoto ni Daudi Were kutoka Kenya, mimi na Ndesanjo Macha wakati wa maswali na majibu. Huyu hapa ni Mwandishi kutoka Zambia, Brenda Zulu, anatutwanga swali. Tazama na picha hii ya Nokia. Hapa Ndesanjo alikamatwa vizuri akisisitiza jambo.

5 comments:

Tanzanian Rant said...

Kaka, Blog yako imetulia, by th way nimepenfda sana jinsi ulivyojiunganisha na flick, am not very good in that but pls nipe ujuzi

Ansbert Ngurumo said...

Tanzanian Rant,
Asante kwa pongezi. Nimejaribu kufungua kwako imekataa. Nilitaka kukueleza kwamba situmii frickr kwa kila picha. Nyingine naweka kutoka kwenye kamera na kompyuta moja kwa moja, na nyingine ni kama hivyo niliyounganisha kwenye hiyo ya Sankofa, kutoka huko ilikochapishwa. Hata hivyo, unaweza kupata mafunzo zaidi kutoka kwenye blog ya Ndesanjo kwenye BLOGGERS' GUIDE. Ipo hapa kwangu, bonyeza ujifunze. Asante.

Anonymous said...

Ngurumo,
Asante kwa kutuletea yanayojiri huko kwa Madiba.Naona wenzako wawili mtandao hauwatendei mema au ndio wanasubiri mambo ya kimya kingi...

Ansbert Ngurumo said...

Jeff,

Nadhani sasa ukiwatembelea utaona waliyoweka. Yapo mengi, lakini kama ujuavyo kazi yaetu ilikuwa kuzungumza, si kujiripoti. Waandishi walioshiriki ndio walituripoti. Mimi nimehojiwa na Redio ya South African Broadcasting (SABC) nikiwa na Ndesanjo (Kwa Kiingereza); nimehojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Channel Africa nayo ya SABC (Kwa Kiswahili); nimehojiwa na waandishi wa Highway Africa News Ageny (HANA); nimehojiwa na wanablogu kadhaa wakiwamo Ramon Thomas wa Afrika Kusini na Sarah Bel wa Uholanzi.

Kwa hiyo, taarifa zipo. Nadhani walivutiwa na jinsi tulivyotetea kazi yetu na hasa lugha yetu. hatuwezi kujisifu, lakini ni dhahiri kwamba hatukuwatia aibu Watanzania waliokuwapo. Hata jina la nchi yetu tumellinda. Fuatilia link hizo nilizokuwekea unaweza kusikia tulichoongea kwenye mahojiano. Naangalia uwezekano wa kuweka hapa Power Point ya mhadhara wangu.

Anonymous said...

Wajameni hongera sana kwa uwakilishi mzuri wa nchi yetu na lugha yetu. Tumewaona na tunawapongeza tena na tena.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'