Monday, September 10, 2007

Hii nayo kali

Zamani Shirika letu la Ndege (Air Tanzania Corporation), kwa sababu ya kutokuwa na huduma inayoaminika, liitaniwa na wabongo, likaitwa Any Time Cancellation (ATC). Wanigeria nao sasa wameibuka na mpya kuhusu 'TANESCO' yao. Kwa sababu ya mgawo wa umeme na matatizo yasiyoisha, mamlaka yao ya umeme iitwayo Nigerian Electric Power Authority (NEPA), imekuwa ikitaniwa na kuitwa Never Expect Power Always (NEPA).

Ili kukabiliana na tatizo la umeme, serikali imeifanyia mabadiliko ya kimfumo, kiutawala na kiuendeshaji, ikaundwa kampuni iitwayo
Power Holding Company of Nigeria (PHCN). Matatizo ya mgawo yamebaki pale pale, na sasa wanaiita Problem Has Changed Name (PHCN).

Sunday, September 09, 2007

Kutoka Grahamstown

Jamaa alinikamata vizuri na kamera yake nilipokuwa nawasilisha mada yangu. Leo Septemba 10. 2007 imekuwa siku ya michakariko. mimi, Ndesanjo na Bob Sankofa tumekuwa tunawasilisha mihadhara yetu kwa wasikilizaji waliokuwa katika Digital Citizen Indaba. Tumejumuika na waandishi wengi kutoka sehemu mbalimbali za Afrika. Hotuba ya ufunguzi wa mjadala wa leo katika Indaba imetolewa na Ndesanjo. Pata sehemu ya mhadhara wa Macha hapa. Nitawaletea taarifa nyingine baadaye. Zoopy wameweka hapa sehemu ya kilichotokea.

Saturday, September 08, 2007

Nimekutana na Ndesanjo

Tayari nimefika Grahamsatown, alasiri Jumamosi Septemba 9, 2007. Nimekutana na Ndesanjo Macha kwa mara ya kwanza, ana kwa ana. Muda wote tulikuwa tunafahamiana kupitia blogu na magazeti. Baadaye jioni tutakuwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Digital Citizen Indaba kama nilivyoeleza hapo chini.

Friday, September 07, 2007

Naenda Bondeni

Wiki hii nitakuwa Bondeni kushiriki mkutano wa Highway Africa na wanahabari wengine kutoka pande mbali za Afrika na kwingineko duniani. Mojawapo ya majukumu yangu huko ni kuzungumzia uandishi mpya wa kijamii katika mkusanyiko ujulikanao kama Digital Citizen Indaba siku moja kabla ya mkutano wenyewe, ambako pia nitashiriki kujadili mada ya kublogu, nikiwa pia na gwiji wa kublogu, mwanablogu nambari wani wa Kiswahili, Ndesanjo Macha na wadu wengine. Msiwe mbali na blogu.

Sunday, September 02, 2007

Asante Lowassa, heko Nyamongo

HII ndiyo nukuu yangu kuu kutoka kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Makamanda wanyeshewa mvua Geita


Mvua haikuwazuia kufanya walichodhamiria. Hii ni sehemu ya umati wa waliohudhuria mkutano wa wapinzani Geita Mjini, Septemba 2).Anayehutubia ni Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
(Picha kwa hisani ya Joseph Senga).

Ndimara Tegambwage afungua blogu


Mwandishi mkongwe wa vitabu na magazeti; mchambuzi mahiri na mjenzi makini wa hoja kali; mmoja wa waasisi wa mageuzi ya vyama vingi nchini; mbunge mstaafu wa Muleba Kaskazini; Ndimara Tegambwage, anayeandika safu ya SITAKI (na hii hapa mpya) katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili, ameingia katika ulimwengu wa blogu. Jina lenyewe la blogu ni dalili tosha kwamba kishindo chake kitakuwa kikubwa.

Wanablogu wengi ninaowajua ni vijana. Wazee wengi wa rika la Ndimara wamekuwa waoga wa teknolojia. Lakini Ndimara hazeeki. Hata katika dotikomu naye yumo. Na kwa wanaomfahamu, Ndimara ni kijana kuliko vijana wengi tulionao, waliozeeka kabla ya wakati wao. Msome hapa.


Mbowe, Zitto watua Mwanza


Wamo katika helikopta hii inayokaribia kutua katika uwanja wa Mirongo, Mwanza, wakiwa na viongozi wengine wa upinzani wanaoandamana nao. Umati wa wananchi, unaishuhudia inavyotua kabla ya mkutano kuanza. (Picha zote kwa hisani ya Joseph Senga)

Mresha katika Chopa ya Mbowe


Mheshimiwa Mrema ameshuka kwenye Chopa, ilipotua katika uwanja wa Mirongo, Mwanza.

Mrema naye atema tete


Mzee wa Kiraracha naye alikuwapo. Hapa anawapa shule wakazi wa Mwanza walioketi chini kumsikiliza.

People's Power


Mbowe 'akiwachochea' wananchi kutumia nguvu ya umma kuishikiza serikali adabu.

Friday, August 31, 2007

Hekalu la Manji?

Bwana ee! Tazama nyumba hii. Lakini Waswahili wanasema imevuka viwango vya kuitwa nyumba. Hili ni Hekalu. Na hizi hapa chini ni sehemu chache za hekalu hilo. La nani? Aliyetuma hizi ni la Yusuf Manji - yule mfadhili wa Klabu ya Yanga; "mgomvi" wa Regi Mengi (na sasa hivi Waislamu kuhusu kiwanja); mfadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); lakini mmoja wa wasomaji wa blogu hii anasema si kweli bali ni nyumba ya Rais Pervaiz Musharaf, mtu aniyejipenda kweli kweli, mchezaji hodari wa Badminton, Jenerali wa Pakistani. Iwe ya yeyote yule, inapendeza na kuvutia. Tazama!

Endelea


Sema mwenyewe


Quite Spacious


Hapa je?


Safi


Chunga, chini panateleza


mh


Mh!


Tuizunguke meza hii


Zungumza, ukichoka pumzika kidogo


Unataka kuogelea?



Labda haya ndiyo Maisha Bora. Tumuulize Kipanya hapo chini!

Thursday, August 30, 2007

Maisha Bora


Nimeipenda katuni hii ya Maosud 'Kipanya.' Wewe je?

Zitto apikiwa kashfa mpya


Habari zilizotapakaa ni kwamba wanamtandao, wakiongozwa na kinara wao, Rostam Azizi, wanapika kashfa mpya dhidi ya Zitto Kabwe (pichani kulia). Eti walitengeneza ya Amina Chifupa ikawalipukia na kuua mtu. Hawakuridhika. Wamejarbu kumdhalilisha Bungeni, akaibuka mshindi. Wananchi wanamshangilia, CCM wakazomewa. Sasa wamesikia Zitto na viongozi wa CHADEMA wanaanza kuzunguka mikoa 10 kuishitaki serikali kwa umma, wanamtandao wanakula njama mpya kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari 'kupika' kashfa mpya. Nia yao ni kupunguza imani ya wananchi na mvuto wa Zitto. Wamekiri, lakini inawauma, kwamba kwa sasa, Zitto amemfunika JK kwa mvuto.

Je, wahariri watakubaliana na mbinu za kina Rostam Azizi? Je, wananchi watamtosa Zitto? Kumkumbatia nani? Je, serikali itabadili sera zake kuhusu madini au itaendelea tu kuhangaika na namna ya kumsakama Zitto?

Tuesday, August 21, 2007

Uchumi ukue, bei zipande hivi?

Waziri Mkuu, Edward Lowassa, anasema uchumi unakua. Lakini wataalamu wanasema bei za bidhaa zinapanda kila siku. Ni ukuaji gani huu wa uchumi? Habari hii imeandikwa na gazeti la serikali, Daily News Agosti 21.08.2007. Soma mwenyewe uone hali ilivyo.

Inflation nears double digits

Overall inflation rate jumped to nine per cent in July, from 5.9 per cent in June, a trend which the National Bureau of Statistics (NBS) attributed to increased food and non-food prices.

“The July 2007 inflation rate has gone up by 3.1 percentage points compared to the June figure,” the Bureau said in a statement made available yesterday. “Some prices for both food and non-food items had gone up,” it added.

Analysts feared the impact of price hikes on the economy, with inflation, a key indicator for consumer comfort and investor confidence, nearly hitting the double digit mark, the highest in more than five years.

The government had for the last three years, targeted to push inflation to a manageable below 4.0 per cent, which could now prove to be quite an uphill task. Before, inflation had nearly dragged the economy to its knees with almost record over 30 per cent rate.

Planning, Economy and Empowerment Minister Professor Juma Ngasongwa told parliament in June that in 2006, average inflation was 7.3 per cent, compared to 5.0 per cent in 2005. In March, this year, inflation was recorded at 7.2 per cent.

The minister attributed the upswing in inflation to increased commodity prices, especially food and petroleum products which also led to high costs of transport and generation of thermal electricity.

The minister expressed optimism on declining inflation after some parts of the country started harvesting food crops, saying in April 2007, the inflation rate had declined to 6.1 percent, from 7.2 per cent registered in March 2007.

NBS said in the statement yesterday that hiked food prices were wheat flour, bread, spaghetti, potatoes and meat. Prices of bananas, fish, cooking oils, beans, cowpeas, sugar and meals in restaurants had also gone up.

It said non-food items that had increased prices were instant coffee, rent, kerosene, electric cookers, sewing machines, kerosene stoves, laundry soap (bar and powdered), scrubbing brush, broom head, tooth brush and hair creams.

Prices that have also gone up include those of car batteries, diesel, petrol, bus fares and private secondary school fees.

However, it noted that prices of clothing, footwear, watches and cell phones had gone down.


Daily News Reporter
Daily News; Tuesday,August 21, 2007 @00:02

Sunday, August 19, 2007

Picha nyingine za Zitto na waandamanaji

Bonyeza hapa uone picha na usome mjadala mwingine mpana.

Habari Leo waua stori ya Zitto Kabwe


Magazeti ya serikali, Sunday News and Habari Leo Jumapili, 'yalikataa' kuandika habari za maandamano na mkutano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, uliofanyika Dar es Salaam Agosti 18 kulaani hatua dhalimu ya Bunge dhidi ya mbunge huyo. AIBU!
Waandishi wao waliyashuhudia maandamano, mkutanoni walikuwepo, lakini walishindwa kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma. UZALENDO uko wapi? Kama wanawadharau hao waliokusanyika kumsikiliza Kabwe, wanamwandikia nani?
Hata hivyo, mpiga picha wao aliweza kumshawishi mhariri wake kutumia walau picha inayoonyesha sehemu tu ya umati uliokusanyika Jangwani kumsikiliza Kabwe. Tazama mwenyewe.

Karamagi anasafiri na mihuri yetu?


KAMA Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, anaweza kusaini mkataba wa madini nje ya nchi, London, Uingereza, wakati yuko ziarani na Rais Jakaya Kikwete, ina maana anasafiri na mihuri yetu? Pata uchambuzi wa swali hili HAPA, na toa maoni yako chini.

Saturday, August 18, 2007

Kishindo cha Zitto Kabwe


Dar es Salaam inazizima. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amegeuka shujaa wa mwaka. Habari kutoka Dar zinasema amekuwa gumzo kila kona, wala mvua nzito haikuweza kuwazuia wananchi kuandamana na kusukuma gari lake kutoka Ubungo hadi viwanja vya Jangwani, Jumamosi, Agosti 18, 2007, alikohutubia mkutano mkubwa na kusema Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisaini mkataba katika Hoteli ya Churchill, London, Uingereza.

Watawala wameduwaa. Bomu walilompasulia Zitto kumdhalilisha limewalipukia wenyewe! Hiki ndicho kishindo kinachozungumzwa. Anasema "tusikumbatie walioshiba" Ipate pia kwa kimombo Hoja kamili na mjadala wake Bungeni HII HAPA. Baadaye, wawekezaji wenyewe, Barrick walijitokeza kutoa maelezo HAYA, lakini Zitto akayachambua pia maelezo hayo na kubainisha uhusiano wa karibu sana kati ya waziri na wawekezaji, huku wakitoa maelezo yanayojikanganya zaidi.

Tuesday, August 14, 2007

Nauliza Kujibiwa

Mpendwa msomaji, nakamilisha mada yangu katika mazungumzo nitakayoshiriki kwenye kongamano la Highway Africa litakalofanyika Septemba 10-12, 2007, Rhodes University, Afrika Kusini. Nimefikiri kwamba ni vema kupata na kutumia mawazo ya wanablogu wenzangu na wasomaji wa blogu hii katika maswali kadhaa ninayojiuliza. Naomba ushiriki wako kwa kujibu maswali yafuatayo kwa kadiri unavyoona inafaa. Nakuhakikishia kwamba nitakapohitaji kutumia mawazo yako mahali popote, nitakunuu bila kuongeza chumvi. Asante. ANSBERT NGURUMO.

1. Kama wewe ni mwanablogu, kwa nini unablogu? Kama si mwanablogu, kwanini unasoma blogu?

2. Je, ni vema wanablogu (na wachangiaji wa maoni) watumie majina yao halisi? Faida na hasara zake ni nini?

3. Je, matumizi makubwa ya blogu yanamaanisha enzi za vyombo vya habari vya kale (redio, magazeti na TV) vimepitwa na wakati?

4. Je, wanablogu wanawajibika kwa nani?

Sunday, August 12, 2007

CCM inaandaa mapinduzi?

MAISHA magumu, kauli na uamuzi tata wa viongozi, mwafaka usiofikika? Vinatupeleka katika mapinduzi mengine? Hilo ndilo swali lwa wiki hii. Soma hapa.

Saturday, August 11, 2007

Wafanyakazi waitolea uvivu serikali


Haijapata kutokea. Terehe 11.Agosti.2007 iliandika historia mpya Tanzania. Wafanyakazi wameandamana na kuilaani serikali ya awamu ya nne kwa kuwadhalilisha, kuwasahau na kuwafanya watumwa katika nchi yao. Ujumbe wao ulifikishwa kwa maandamano, nyimbo, mabango na hotuba kali. Gazeti la Mwananchi Jumapili linaripoti hivi:

Wafanyakazi wampa Rais Kikwete siku 30

*Wamtaka Katibu wao kumwona na kurejesha majibu
*Wadai matumizi ya sheria kudai haki yameshindikana
*Walalamikia mishahara ya wabunge na ununuzi wa mashangingi

WAFANYAKAZI mkoani Dar es Salaam, wamempa siku 30 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nestory Ngulla, kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete na kurejeshewa majibu, kuhusu nyongeza duni ya mishahara, ili kuepusha hatua nyingine watakazotumia kudai mishahara.

Tamko hilo lilitolewa na wafanyakazi hao kupitia risala yao iliyosomwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vyama 18 vya wafanyakazi nchini kupinga kima cha chini cha mshahara wa serikali, kilichopitishwa na bunge hivi karibuni.

Baadhi ya vyama hivyo, ni pamoja na cha Walimu (CWT), Sekta ya Afya (Tughe), Migodi, Nishati, Ujenzi (Tamico), Serikali za Mitaa (Talgwu), Mabaharia (Tasu), Walinzi binafsi (Tupse), Mashambani (Tpawu), Shughuli za Meli (Dowuta), Mawasiliano (Tewuta), Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Waandishi wa Habari (TUJ) na Chodawu.
Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wafanyakazi hao, Katibu wa Raawu, Kanda ya Mashariki, Evarist Mwalongo alisema wamefikia hatua hiyo wakiamini kwamba, matumizi ya kisheria kudai mishahara yatawafikisha katika hali mbaya.

"Hali hiyo itakuwa imelazimishwa na serikali. Wafanyakazi hatutaki kufikia hali hiyo kwani Uhuru wa nchi hii tuliutolea jasho sisi wenyewe," alisema Mwalongo na kushangiliwa na umati wa wafanyakazi waliohudhuria mkutano huo.

Mwalongo alisema, wafanyakazi mwaka huu, wanadai nyongeza ya mishahara kutokana na kukithiri kwa shida baada ya nyongeza hiyo kulimbikizwa kwa miaka zaidi ya 13 iliyopita, hali ambayo imesababisha makali ya maisha kutovumilika tena.

Kutokana na hali hiyo, alisema serikali imekosa huruma na kuacha kutambua kuwa wafanyakazi nchini ndio waliodai Uhuru wakisaidiana na wakulima, badala yake imekuwa ikiwajali wafanyabiashara peke yake kwa kuwafanya kama ndio mhimili wake wa kusimamia sera, uchumi na siasa za nchi.

Mbali na hilo, Mwalongo alisema serikali imefikia kupuuza hata sheria zilizotungwa kusimamia na kulinda masilahi na masuala ya wafanyakazi.

Alisema inasikitisha kuona Wizara ya Utumishi chini ya Waziri wake, Hawa Ghasia, imeamua kudharau sheria namba 19 ya mwaka 2003 inayohusu majadiliano na vyama vya wafanyakazi kupanga mishahara ya watumishi wa serikali.

"Mheshimiwa Ghasia ameamua kupuuza utawala wa sheria na kuanza ukurasa mpya. Amepanga mishahara ya watumishi kadri alivyoona yeye kutoka Sh75,000 hadi Sh84,000.
Mshahara wa Sh84,000 unakatwa kodi ya Sh 600 kama kodi ya PAYE na akiba ya uzeeni Sh8,400, zinabaki Sh 75,000 ambazo ndiyo mshahara wa zamani.

"Mshahara huo ukigawa kwa Sh 30 utaona mfanyakazi ataishi kwa Sh2,500 kila siku ambazo zitumike kama matumizi mengine ya lazima kila siku. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana vyama vya wafanyakazi vilipendekeza kima cha chini kiwe Sh315,000 sawa na Sh10,500 kwa siku," alisema Mwalongo.

Alisema inasikitisha pia kuoana Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana chini ya Waziri wake, Kapteni John Chiligati, imeamua kulala usingizi kwa kutosimamia sheria namba 6 ya mwaka 2004 inayotakiwa kuunda Baraza la kupanga kima chini cha mishahara kwa ajili ya sekta binafsi ambako kuna hali mbaya kupindukia kwa kuendelea kupata mshahara wa Sh48,000 tangu mwaka 2002.

"Sisi wafanyakazi hatuelewi kama serikali ipo kwa ajili ya Watanzania kwani kwa mshahara wa Sh84,000 ukigawa kwa Sh10,500 kama matumizi kwa mahitaji ya lazima ya kila siku utadumu siku nane na kama mfanyakazi atakula mlo mmoja kwa siku utadumu siku 16 tu.

"Mshahara huo wa Sh84,000 ni asilimia 50 au nusu ya posho ya mbunge anayopata katika kikao cha siku moja na mshahara wa mbunge wa mwezi mmoja ambao ni Sh1,500,000 unaweza kumlipa mfanyakazi huyo kwa miezi 17.

Uchambuzi kama huu ukiwekwa watumishi wa kima cha Sh84,000 inasikitisha kiasi cha kujenga hasira mbaya katika jamii ya Watanzania," alisema Mwalongo.

Alisema pamoja na shida za mishahara duni, serikali imetengeneza mzigo mzito unaotokana na bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2007/08, iliyokuja na kodi kubwa katika mishahara, mfumuko wa bei uliotokana na bei kubwa ya mafuta ya dizeli, petroli na vilainishi vya mitambo na kwamba, usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani umekuwa pia gharama kubwa inayowatesa wafanyakazi maradufu.

"Kukosekana kwa vyombo vya usafiri, suala hili halishughulikiwi na serikali kwa vile wakuu wote wanatumia magari ya gharama za kutisha yanayowalaza usingizi wasione kuna nini kwa wananchi. Inasikitisha kuona kiongozi anapita na VX ya Sh150 milioni bila hata ya huruma kwa mtoto au watoto wa shule kama hapendi kuwapa msaada wafanyakazi wenzie ingetosha kuwaonea huruma watoto wa shule.

"Gari aina ya VX moja ingeweza kununua gari la kubebea wafanyakazi zaidi ya 100. Mfano huu ukizidishwa kwa namba ya magari ya mawaziri na watendaji wakuu wa serikali yetu utaona serikali inao uwezo mkubwa sana wa kugawa mshahara wa kuishi wa Sh 315,000 bila kikwazo," alisema Mwalongo.

Alisema mishahara midogo wanayolipwa wafanyakazi, inaleta uhafifu katika malipo ya uzeeni kwa wastaafu ambao wametumikia serikali kwa uadilifu mkubwa.

Mwalongo alisema bila kujali kuwa mishahara ni midogo, serikali bado inaendelea kuwaonea wafanyakazi kukopa kwa nguvu jasho la wanyonge, kwa kulimbikiza madai ya nauli, likizo, malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi, kama vile walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watumishi wengine wa manispaa na mashirika mbalimbali.

Alisema wakati hali ikiwa hivyo, soko la ajira limetekwa na wageni kwa visingizio na kejeli dhidi ya wafanyakazi wazalendo, kwamba Watanzania ni wavivu, wazembe, hawajui Kiingereza na kadhalika.

"Inasikitisha wanaotoa kauli hizo ni Watanzania wenzetu bila kutambua kuwa dawa za kutibu uzembe, uvivu na kutojua Kiingereza ni malipo mazuri, mbona Watanzania wanang'ang'aniwa nchi za nje kwa bidii ya kazi na kuzungumza Kiingereza chenye fasihi tamu?

"Tunasema waache kutukejeli kuanzia sasa, iwe mwisho kuuza nafasi zetu za kazi ovyo, waone aibu wawekezaji wao wameanza kuwekeza mpaka katika vibanda vya kukaanga viazi na maua ya plastiki, watainuaje uchumi wetu?" alihoji Mwalongo.

Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo mishahara haitaongezwa italeta athari kubwa, ikiwamo wafanyakazi kushindwa kushiriki katika vita dhidi ya rushwa, kiwango cha umaskini kitakithiri katika jamii, kipindupindu, ujinga, kukosekana tija ya taifa na nidhamu ya kazi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhadhiri Mstaafu wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, aliishangaa serikali kuona ikikataa kutambua kwamba, wananchi hivi sasa wanakabiliwa na kipindi kigumu kutokana na kujenga mgawanyiko na mpasuko katika jamii ya Watanzania.

"Kuna kundi la matajiri na maskini, tuna tabaka la walala heri na walala hoi. Kama tutaendelea katika mwelekeo huu kwa kasi, tutajikuta tuna mataifa mawili," alisema Profesa Shivji na kushangiliwa na umati wa wafanyakazi waliohudhuria mkutano huo.

Katibu wa Kanda ya Dar es Salaam wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi nchini (Cotwu), Buhari Semvua, akizungumza katika mkutano huo, alipinga msimamo wa serikali wa kuendelea na majadiliano Septemba, mwakani na wafanyakazi kuonya kuwa iwapo serikali itapuuza malalamiko yao nchi haitakalika.

"Hatukubali hiyo mwakani na wajue kuwa wananchi wakikata tamaa, hatua watakazochukua, patakuwa hapakaliki, hapatoshi. Siku 30 tusipojibiwa, hizi (maandamano) za leo ni rasharasha," alisema Semvua.

Naye Ngulla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka wafanyakazi kutobabaishwa na wabunge na kuahidi kwamba, atahakikisha anafikishia serikali malalamiko yao ndani ya muda aliopewa.

Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano ya wafanyakazi hao yaliyoanzia katika Ofisi za Makao Makuu ya Tucta, Mnazi Mmoja saa 2:00 asubuhi na kupita katika Barabara za Bibi Titi Mohamed na Morogoro na kuishia katika Viwanja vya Jangwani, huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kuilaani serikali.

Baadhi ya mabango yalisomeka: "Walalahoi Sh84,000 kwa mwezi, mbunge Sh120,000 kwa siku, haki iko wapi?" "Mshahara huishia nauli ya daladala, vigogo kwenye mashangingi, kima cha chini kiongezwe, hii ni haki", "Mishahara iendane na hali halisi ya uchumi wa nchi kwa sasa", "Bila walimu Rais Kikwete ungekuwa wapi? Mbona hutukumbukwi?"

"Nauli za likizo hazitolewi kwa wakati kwa nini? Walimu tunateseka", "Haturidhiki na waraka mpya wa mshahara", "RAAWU Taasisi ya Watu Wazima. Kwa ari hii, kasi hii, nguvu hii na mishahara hii ya wafanyakazi tumekwisha!" "Kuna siri gani kati ya sekta binafsi na serikali kuhusu mishahara?"

Mbali na mabango hayo, waandamanaji hao walikuwa wakiimba kwa kusema: "Na sisi hatulali, bado mapambano, mpaka kieleweke", "Kilio, kilio, kilio, tutamlilia nani?"

Sunday, August 05, 2007

Sunday, July 22, 2007

Tanzania isiyo na UKIMWI inawezekana?

Soma hapa.

Serikali Kupinduliwa

HABARI hii ilileta kizaazaa kati ya serikali na gazeti la MwanaHALISI Jumatano 18.07.2007. Serikali inagombana na maoni ya wakili na mwanasiasa maarufu, mmoja wa waasisi wa mageuzi ya kisiasa nchini, Mabere Nyaucho Marando.

Marando anasema serikali inaweza kupinduliwa, iwapo wananchi watajua haki zao.

“Wewe unatumia lugha ya kupindua. Kwa lugha ya kawaida, kupindua ni kutumia nguvu za kijeshi. Lakini yapo mapinduzi mengine yanayowezekana. Ni yale yanayotokana na mwamko wa wananchi,” amesema.

Katika mahojianao maalum na MwanaHALISI juu ya miaka 15 ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, Marando amesema, “Wananchi wana uwezo wa kuipindua serikali kupitia njia halali ya sanduku la kura.”

Akihusisha hasa na madai ya wabunge wa CCM, Job Ndungai na Janet Masaburi wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwamba elimu inayotolewa na HakiElimu inaweza kusababisha serikali kupinduliwa, Marando alisema:

“Hili linawezekana kabisa. Kinachohitajika ni mwamko zaidi kwa umma. Wananchi wakipata mwamko, wanaweza kuipundua serikali kwa njia ya kura.
Marando amesema serikali ya sasa imeshindwa kuwajibika na hivyo inaweza kung’olewa kwa nguvu za umma.

Amesema HakiElimu inafanya kazi nzuri na inaifanya vizuri na kwamba vyama vya upinzani havina budi kujifunza kutoka HakiElimu, hasa katika suala la utafiti wa hoja muhimu za haki za binadamu na maslahi ya jamii.

“Unajua, CCM inaumwa ugonjwa wa kusinyaa. Ugonjwa huu huvipata vyama vilivyokaa madarakani kwa muda mrefu. Chama kikikaa madarakani kwa muda mrefu, kinasinyaa. Kinakuwa na mchoko,” anasema.

Katika mahojiano ambayo yamechapishwa katika toleo hili, Marando anasema, sababu za kuchukia CCM bado zipo, “Hiki bado ni chama cha kidkteta. Matumaini ya wananchi bado yapo, kwamba kuna siku watajikomboa kutoka udikteta huu.”

Kuhusu mafanikio ya upinzanai katika kipindi hiki, Marando anasema, “uwanja wa demokrasia umepanuka. Serikali inachukua hatua, japo kwa kiwango kidogo na bila upinzani serikali ingefanya itakavyo. Siridhiki, lakini angalau tumepata mahali pa kuanzia.”

Alipoulizwa CCM inaweza kujivunia nini katika miaka hiyo, Marando alisema, “Wanaweza kujivunia bahati yao nzuri ya kushikilia madaraka bila kuwa na sababu za msingi za kutawala na kuendelea kubaki madarakani wakati hawastahili kuwapo.”

Marando amesema CCM haina zaidi cha kujivunia, “Labda ujinga wanaowalisha kwa Watanzania kwamba CCM ndiyo baba na ndiyo mama, wakati si kweli. Wanaweza kujivunia pia rushwa ambayo wameifanya kuwa sera ndani ya CCM na serikali yake. Basi!”

Kuhusu uwezo wa vyama vya upinzani kifedha, Marando anasema, ni kweli vyama havina fedha wala wafadhili, “Lakini lazima wafanye kazi hiyo. Waende kwa Watanzania wenzao… kuomba msaada. Hilo ni jukumu lao na hawawezi kulikwepa hata kidogo.”


Soma Mahojiano na Marando

MwanaHALISI, Serikali wakaribia kuzichapa

Serikali ya awamu ya nne bado inaendelea kukosa uvumilivu. Huku rais Jakaya Kikwete akidai haogopi kukosolewa, matendo ya serikali yake yanaonyesha tofauti. Baada ya kulikosakosa Tanzania Daima mara kadhaa, sasa imeamua (kwa mara nyingine) kulivalia njuga gazeti la kila Jumatano la MwanaHALISI. Soma hapa. Kutokana na sakata hilo, Mchambuzi na Mwandishi mkongwe, Ndimara Tegambwage, anaipatia serikali TUISHENI ya bure.

Sunday, July 15, 2007

Marais wastaafu wafe au washitakiwe?

Rais mstaafu anapokufa taifa haliyumbi. Lakini wapo wanaosema kwamba akishitakiwa kwa makosa aliyofanya akiwa madarakani taifa litayumba. Hii ni kweli au kuna linalofichwa nyuma ya hoja hii? Soma mjadala.

Sunday, July 01, 2007

Amina aliiogopa CCM kuliko wauza mihadarati

Alisema: "nawajua ni watu wa namna gani...wanaweza kunidhuru...”

Buriani Amina Chifupa; umekwenda kishujaa




Na Ansbert Ngurumo, Hull
1.
Amina Mpakanjia;
Nani asiyekujua?
Nani hajakusikia?
Nani hakukutambua?

2.
Eti umetukimbia?
Sikubali nakataa;
Nani kakuondoa?
Lipi umemfanyia?

3.
Amina, mi siamini;
Kwamba tena sikuoni;
Haraka hiyo ya nini?
Wakimbia ‘fanya nini?

4.
Najua hukuwa radhi;
Kwenda chini ya aridhi;
Yatoka wapi maradhi;
Bila idhini ya Kadhi?

5.
Bado ulikuwa dogo;
Miongoni mwa vigogo;
Yako marefu malengo;
Sasa wayapa kisogo.

6.
Umekwenda kwa lazima;
Siku zote tutasema;
Umeondoka mapema;
Nani amekusukuma?

7
Mungu ndiye anajua;
Kwanini watangulia;
Ameshindwa kuzuia;
Majonzi ya Tanzania.


8
Kama angetuuliza;
Nani kumtanguliza;
We tusingekupoteza;
Kura tungezipunguza.


9
Si wewe mwenye hatia;
Ulopaswa tangulia;
Wapo walokuvizia;
Sasa umewakimbia!

10.
Wapo waliokubeza;
Mwenyewe ukanyamaza;
Pole pole ukaanza;
Hadi wao kushangaza.

11.
Kisomo chako kidogo;
Si kama chao vigogo;
Kiliyabeba magogo;
Kuwaachia usongo.

12.
Woga ‘liweka pembeni;
Na nchi yako usoni;
Lionekana makini;
Kama vile wa zamani.

13.
Vijana uliwawaza;
Hata wale wasocheza;
Sumbawanga hadi Mwanza;
Ulisema: ‘hawa kwanza.’

14.
Soka ulishangilia;
Timu yetu saidia;
Nguvu kuiongezea;
Us’okuja shuhudia.

15.
Watoto ulitetea;
Kama mama asilia;
Ulijua Tanzania;
Hao yawategemea.

16.
Yatima ‘lisaidia;
Tumaini ‘liwatia;
Wagonjwa ‘lisalimia;
Wote uliwawazia.


17.
Tabasamu lilijaa;
Huruma lilichochea;
Urembo ulitumia;
Wengi kuwahudumia.

18.
‘Liitwa Mama shughuli;
Kwa kazizo mbalimbali;
Hata kuwapamba wali;
Mambo yako kali kali.

19.
Kikwete anauliza;
Sitta huyo kanyamaza;
Chifupa amepoteza;
Nani ‘tambembeleza?

20.
Wapo ul’oshambulia;
Kwa haki nakutetea;
Mihadarati bugia;
Hukutaka kusikia

21.
Nyota yako iliwaka;
Hata kwa wasoitaka;
Haya sasa umetoka;
Lije walilolitaka?

22.
Sadaka uliyotoa;
Sote tunaitambua;
Hata walokusumbua;
Hili watalijutia.

23.
Hatuwezi simangana;
Sasa twafarijiana;
Ila twaweza ‘onyana;
Hata kushauriana.

24.
Amina umetoroka;
Waacha moto wawaka;
Umejitoa sadaka;
Tutakayoikumbuka.

25.
Twajua ‘metangulia;
Sote tutaelekea;
Ila moja twatambua;
Umekwenda kishujaa!

26.
Umekimbia kwa kasi;
Kuliko hata ya fisi;
Vijana watakumisi;
Wabunge hata na sisi.

27.
Kina mama wanalia;
Mwenzao wakumbukia;
Wasanii nao pia;
Nyimbo wanakuimbia.

29.
Maisha yako twakiri;
Ni mafupi na ya heri:
Marefu yaliyo shari;
Umeachia wapori.

30.
Tulia na Malaika;
Pale atapokuweka;
Tabasamu cheka cheka;
Yametimu, yamefika.

31.
Ukiukuta mpira;
Cheza na Hawa na Sara;
Shambulia mduara;
Hata mbinguni, ahera.

32.
Mpakanjia na mwana;
Baba na Mama Amina;
Kubali ya Maulana;
Itikieni: Amina.

Thursday, June 28, 2007

Sunday, June 24, 2007

Nauli nafuu kwenda popote

Ni kama tangazo vile, lakini ni huduma muhimu kwa wasafiri. Soma hapa.

Uzalendo wa Meghji unatia shaka

Tuhoji upeo wa Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, katika suala la uzalendo.

Wednesday, June 20, 2007

Furaha ya Stars, ulevi wa watawala

Watawala wetu wanataka kufunika machungu ya bajeti ya serikali kwa chereko za ushindi wa Taifa Stars dhidi ya Burkinafaso? SOMA HAPA

Sunday, June 03, 2007

Watanzania wataacha lini kuwashabikia 'manabii'?

'Nabii' mmoja wa Tanzania aliyedai ametokewa na Roho Mtakatifu, alioa wanawake wote kijijini kwake, akazaa nao watoto 59 ambao hakuwasomesha! Aliwaahidi wafuasi wake kwamba wangepaa kwenda mbinguni baada ya miaka 70, akafa kabla ya unabii wake kutimia. sasa limekuwa zogo. Watanzania tunapata somo gani? SOMA hapa.

Wednesday, May 30, 2007

Wanamtandao waanza kunijibu

Wa Kwanza amesema hivi. Kwa bahati ya ajabu, alikutana na makala yangu inayomhoji yeye binafsi na wenzake siku hiyo hiyo, katika gazeti hilo hilo. What a coincidence! Majibu yangu kwa baadhi yao ni haya.

Monday, May 28, 2007

Tumeshindwa Real Madrid, Tutaweza MKUKUTA?

REAL Madrid 'imetema' mwaliko wa JK. Ina maana gani? Soma UCHAMBUZI HUU.

Sunday, May 20, 2007

Serikali ishindwe, mamluki waweze?

KUNA mkakati mpya wa 'kazi' uliobuniwa na baadhi ya viongozi wa serikali yetu pale wanaposhindwa kujibu hoja za wakosoaji zinazoibuliwa katika vyombo vya habari. Hawatoi majibu, lakini wanaandaa mamluki kushambulia wakosoaji wa 'wakubwa.' Serikali iliyoanzia magazetini, imerudi tena magazetini? Mamluki hawa wanaweza kutoa majibu ya serikali? Serikali yenyewe inafanya nini? Soma UCHAMBUZI HUU, na toa maoni yako.

Sunday, May 13, 2007

Mwanza ina nini na Rais Kikwete?

Kwanza kuvamiwa jukwaani; pili mapanki; na sasa Chitalilo. Kwa NINI?

Wednesday, May 09, 2007

Karibu Katika Nyumba Mpya

Kwa sababu za msingi kabisa, nami nimejenga nyumba mpya mpya. Wengine wanasema ni kiota. Unataka kuingia? Bofya hapa

Sunday, May 06, 2007

Kina Chiluba Wengi Afrika

Tunazungumzia kupiga vita rushwa? Zambia imetoa mfano na funzo kwetu. Nasi Tanzania tunao kina Chiluba wengi. Badala ya kuwachukulia hatua tunawalinda. BOFYA HAPA.

Sunday, April 29, 2007

Boyz II Men wanaogopa kuitwa wasanii?


Soma Maswali yangu kwa serikali ya JK inayong'ang'ania kufuga na kutisha vyombo vya habari na wanahabari. Hii Hapa.

Thursday, April 12, 2007

Watawala wafe, taifa lifufuke

Hizi ndizo salaam zangu za Pasaka mwaka huu 2007 kwenu wasomaji. Zipo HAPA.

Sunday, March 18, 2007

Inatekenya mbavu, au vipi?




MARA moja moja ni vema kujiburudisha kidogo, kucheka, kulegeza misuli na kupunguza tension. Katuni hii imetumwa kwangu na Peter Nyanje, ambaye ameipokea kutoka kwa wengine katika mzunguko wa kutumiana vichekesho. Nikaona vema niipatie mahali pa kutulia, ili wasomaji wa blogu hii, hasa wale ambao hawakupata na hawatapata 'bahati' ya kutumiwa katuni hii, nao wapate uhondo huu. BOFYA kwenye picha usome maelezo yake.

Monday, March 12, 2007

Makala za kihistoria juu ya Chifu Marealle

Historia ni mama wa elimu yote. Zisome makala hizi mbili, utakiri hii ni sehemu nyeti ya historia yetu, katika nafsi ya Hayati Chifu Thomas Marealle. Anza na hii ya Kibanda, halafu malizia na hii hapa ya Halimoja.

Sunday, March 11, 2007

Friday, March 09, 2007

Eti Pombe ina homoni za kike?

Hii imenifikia katika mzunguko wa kutumiana meseji za utani, nikaona niiweke hapa kwa faida ya wasomaji. Nadhani huu ni utani tu, usioweza kusababisha ugomvi kwa wanaharakati wa jinsia.

Last month, National University of Lesotho scientists released results of a recent analysis that revealed the presence of female hormones in beer. Men should take a concerned look at their beer consumption. The theory is that beer contains female hormones (hops contain phytoestrogens) and that by drinking enough beer, men turn into women. To test the theory, 100 men drank 8 pints of beer each within an hour period. It was then observed that 100% of the test subjects:

1) argued over nothing.
2) refused to apologize when obviously wrong.
3) Gained weight.
4) Talked excessively without making sense.
5) Became overly emotional.
6) Couldn't drive.
7) Failed to think rationally
8) Had to sit down while urinating.

No further testing was considered necessary.

Wednesday, March 07, 2007

TUENDAKO: Uchambuzi Bora kwa miaka 10

Nimesoma makala nyingi za Kibanda, kwa miaka 10 iliyopita. Ni mwandishi mzuri na makini. Lakini sijawahi kusoma makala yake nzuri kuliko hii hapa. Ameikuna akili yangu. Bofya hapa chini usome mwenyewe.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/3/7/makala7.php Soma pia nondo za Kibanda kwa JK katika mfululizo wa makala za TUENDAKO.

Sunday, March 04, 2007

Tukubaliane, hatuna Wimbo wa Taifa

Unajua kwamba Watanzania hatuna Wimbo wa Taifa? Bofya hapa uone sababu.

Saturday, March 03, 2007

Zama mpya, majibu ya kizamani

Majibu ya kizamani, zama mpya! Inakubalika? Bofya hapa.

Thursday, February 22, 2007

Soksi za Rais Zimetoboka: Vidole Vinachungulia

World Bank President Paul Wolfowitz may be dedicated to freeing the world from poverty - but he seems unable to afford a new pair of socks!!Mr. Wolfowitz's sartorial deficiencies were revealed when he took his shoes off while visiting a mosque in Edirne, western Turkey. The guy's torn socks were there for all to see!!......By the way, zako zikoje leo!!? For records purposes, the last World Bank annual report, for 2006, puts the president's salary as of 1 July, 2005, at $391,440 (£200,279)....... An almost/equivalent of Tshs. 300,020,925 per month!!........

(Imetumwa kwangu na mtu aliyekuwa anaizungusha kwa marafiki)

Monday, February 19, 2007

'Mchemsho' wa Uhuru: Uingereza yawa Marekani


JUMAMOSI Februari 17, 2007 Rais Jakaya Kikwete alikuwa nchini Uingereza na alikutana na badhi ya Watanzania waishio nchini humo na kuzungumza nao. Cha kushangaza, gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni mwenyekiti, lilitumia picha zake na kuwaeleza Watanzania na dunia nzima kwamba Rais alikuwa Marekani, na kwamba Balozi wa Tanzania nchini Marekani ni Mwanaidi Maajar. CAPTION ya picha unayoona hapa iliyotumika katika tovuti ya gazeti la Uhuru 19.02.2007 ilisema hii:
RAIS Jakaya Kikwete akisisitiza jambo alipozungumza na Watanzania waishio Marekani, kwenye hoteli ya London's Royal, juzi Kushoto ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mwanaidi Maajar. (Picha na Freddy Maro).

Sunday, February 18, 2007

Ndiyo. Tuchukie, Tuchukue Hatua

Ndesanjo ametema cheche katika gazeti la Mwananchi Jumapili Februari 18, 2007. Makala yake niliiunganisha hapa, lakini baada ya Jumapili kupita, ikawa haipatikani tena. Sasa ukibofya, inakuja nyingine mpya; nikaamua kuhariri na kuiondoa. Nadhani wataalamu wa tovuti ya Mwananchi wanapaswa kujua kuwa tovuti yao haitunzi kumbukumbu za nyuma; warekebishe kasoro hiyo. Lakini hoja ya Ndesanjo ni kwamba Watanzania wasiwe wanachukia tu maovu ya watawala wao, wanalalamika, halafu uchaguzi ukifika wanawarejesha madarakani. Wawaondoe. Anasema ni vema waanzie kwenye serikali za mitaa, si Ikulu tu. Makala inasisitiza kile ambacho mwandishi mwingine, Ndimara Tegambwage, hupenda kukiita 'kuchukia na kuchukua hatua.' Kama unaweza itafute uisome mwenyewe. Ni tamu!

Saturday, February 17, 2007

Sijanuna; natafakari

Usitazame glasi. Mtazame huyo anayekutazama, mwenye glasi. Unaweza kumtambua katika picha ya pili? Hiyo ilikuwa Novemba 11, 2006 baada ya mkutano na mafunzo ya uandishi wa habari za sayansi ulioandaliwa na kudhaminiwa na Shirikisho la Waandishi wa Habari za Sayansi duniani (WFSJ), 4-10 Novemba, 2006 Nairobi, Kenya. Nilirejea UK kesho yake. Washiriki wengine, katika matukio tofauti, wapo hapo chini. Picha kwa hisani ya WFSJ.






Tuesday, February 13, 2007

Mbiki Shujaa

Mrembo Mbiki Msumi ameamua kuwa shujaa. Apongezwe; aungwe mkono. Soma hapa.

Sunday, February 11, 2007

Ya Lowassa kama ya Sumaye?

Usishangae. Boksi hilo limejaa pesa taslimu. Lakini hiyo si hoja yangu hapa.
INASEMEKANA kuwa rada iliyonunuliwa na Tanzania kwa bei ghali, na ambayo inanuka rushwa, sasa ni mbovu. Ndege ya Rais, yenye utata na kunuka rushwa pia, haitumiki ipasavyo na inazidi kutafuna mabilioni ya wanyonge. Sasa limeibuka hili la magari ya kifahari ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Kwanza ni ya bei mbaya; lakini si ya lazima. Zaidi ya hayo, wataalamu wanasema hayafai! Kwa mara nyingine, tumeliwa! SOMA HAPA. Hata Frederick Sumaye alianzwa hivi hivi.

Tunaelekea kujifananisha na Nduli Idi Amin

VINGOZI wetu wameanza pole pole kwenda mwendo wa ki-Amin Amin. Tunawaeleza, hawasikii. Au wanasikia lakini ndiyo hulka yao? Ona sasa tunaanza kuwafananisha na Amin.

This is why we see some boiled seeds sprouting


This message was forwarded to me by a friend, who also received it from someone else. I have posted it here so as to expose it to readers of this blog. It is a never miss. Want to prove me wrong? Read on.



An aging king woke up one day to the realisation that should hedrop dead, there would be no male in the royal family to take his place. He was the last male in the royal family in a culturewhere only a male could succeed to the throne - and he was aging. He decided that if he could not give birth to a male, he would adopt a son who then could take his place but he insisted that such an adopted son must be extraordinary in every sense of the word. So he launched a competition in his kingdom, open to all boys, no matter what their background. Ten boys made it to the every top. There was little to separate these boys in terms of intelligence and physical attributes and capabilities.


The king said to them, “I have one last test and whoever comes top will become my adopted son and heir to my throne.” Then he said, “This kingdom depends solely on agriculture. So the king must know how to cultivate plants. So here is a seed of corn for each of you. Take it home and plant and nurture it for three weeks. At the end of three weeks, we shall see who has done the best job of cultivating the seed. That person will be my heir-apparent.” The boys took their seeds and hurried home. They each got a flower pot and planted the seed as soon as they got home. There was much excitement in the kingdom as the people waited with bated breath to see who was destined to be their next king. In one home, the boy and his parents were almost heartbroken when after days of intense care, the seed failed to sprout.


He did not know what had gone wrong with his. He had selected the soil carefully, he had applied the right quantity and type of fertilizer, he had been very dutiful in watering it at the right intervals, he had even prayed over it day and night and yet his seed had turned out to be unproductive. Some of his friends advised him to go and buy a seed from the market and plant that. “After all,” they said, “how can anyone tell one seed of corn from another?” But his parents who had always taught him the value of integrity reminded him that if the king wanted them to plant any corn, he would have asked them to go for their own seed. “If you take anything different from what the king gave you, that would be dishonesty. Maybe we are not destined for the throne. If so, let it be but don’t be found to have deceived the king,” they told him. The d-day came and the boys returned to the palace each of them proudly exhibiting a very fine corn seedling. It was obvious that the other nine boys had had great success with their seeds. The king began making his way down the line of eager boys and asked each of them, “Is this what came out of the seed I gave you?” And each boy responded, “Yes, your majesty.” And the king would nod and move down the line.


The king finally got to the last boy in the line-up. The boy was shaking with fear. He knew that the king was going to have him thrown into prison for wasting his seed. “What did you do with the seed I gave you?” the king asked. “I planted it and cared for it diligently, your majesty, but alas it failed to sprout.” The boy said tearfully as the crowd booed him. But the king raised his hands and signalled for silence. Then he said, “My people, behold your next king.” The people were confused. “Why that one?” many asked. “How can he be the right choice?” The king took his place on his throne with the boy by his side and said, “I gave these boys boiled seeds. This test was not for cultivating corn. It was the test of character; a test of integrity. It was the ultimate test. If a king must have one quality, it must be that he should be above above dishonesty. Only this boy passed the test. A boiled seed cannot sprout.”


We live in a society that has become obsessed with success and many show success at any cost. We say the end justifies the means. It is the tragedy of life. You see, failure often is an invitation to God to show that he is all powerful and does not need help to make us great or to bless us. You know, sometimes God looks for people who will trust him completely no matter what so he could show the world that it is not by might or by power but by his spirit. Failure is sometimes ordained by God. But many seek to circumvent divinely ordained failure by resorting to dubious means.


When a civil servant builds a big house and sends his five children to expensive schools when hedoes not have a second source of income, is that not a case of a boiled seed sprouting? When a minister of state is able to sustain a lavish mistress and at the same time put up houses from his income as minister, is that not a case of a boiled seed coming to life? We should stop cheering rogues in this world.


I believe that not all marriages are meant to have children. I believe that some women would stand before God with their children and God would say, “That’s strange. I did not give you and your husband children so how did you get these?” I believe that not every student should make it to the university. So, many would stand before God with their certificates and God would say, “Now that is strange. How did you get to the university when I closed the door to the university to>you?” I believe that not all people are supposed to marry. But there are those who would throw away their scruples just to get a spouse. Now before God’s judgement throne, they would hear, “Now that is strange. You were to remain single to honour my name. So how did you get a spouse when I did not give you one?”


The Bible says the race is not for the swift and the battle is not for the strong. So, how come, that in this world, the swift wins the race and the strong the battle?


Boiled seed does not sprout.

Monday, February 05, 2007

GARI HILI LINAUZWA


Nimepokea mzigo huu kutoka kwa watu, nikaona niuweke hapa labda atapatikana mteja; nami niambulie kamisheni!

Maelezo yake haya hapa kwa Kiingereza:

TOYOTA HILUX FOR SALE
* Metallic blue
* 5 Passengers
* 6 Cylinder power
* Customised Suspension
* Engine Noise completely harnessed
* KAR registration
* Efficient fuel consumption 10ml/bm

Serikali kuua 'chuo' hiki?


Iruhusiwe? Iachwe ifanye itakalo kunyonga bongo za Watanzania? Huyu HATAKI. Wewe je?

Sunday, February 04, 2007

Huu ni ushindi wa wadau?

NAONA serikali imetambua uchafu wa muswada wa uhuru wa habari unaopingwa na wadau wengi nchini. Imeamua kurudi kwa wadau. Ngoja tusubiri staili mpya ya serikali ya kuwatambua, kuwapata wadau hao, na kuwasikiliza. Soma stori hii.

Bado kuna mengi mbele ya CCM

Mengi yapi hayo? SOMA HAPA

CCM haina cha kusherehekea



Mwandishi mkongwe Yusuf Halimoja anatukumbusha kuwa Mwalimu Julius Nyerere (pichani juu), mwasisi wa CCM, alisema chama hicho kilianzishwa kujenga ujamaa, kulinda heshima ya Tanzania na kuwatetea wakulima na wafanyakazi. Baada ya miaka 30, je, kimefanikiwa? CCM ina cha kusherehekea? PATA JIBU.

Miaka 30: Hukumu ya CCM


Uchambuzi huu murua, ulioandikwa na Mwandishi Wetu wa gazeti la Mwananchi, umechukuliwa kutoka gazeti la Mwananchi Jumapili, Februari 5, 2007 ukiwa na kichwa cha habari MIAKA 30 CHAMA TAWALA KIMESAHAU NGUZO ZILIZOKIJENGA. Kweli. Tukiihukumu CCM kwa miaka 30 ya umri wake, tuna kila sababu ya kukubaliana na mwandishi huyu. Endelea.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), leo kinaadhimisha sherehe za kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Mengi yamezungumzwa kuhusu historia ya chama hiki, lakini kubwa ni kuwa, sasa CCM imegeuka na kuacha nguzo zilizo katika bendera yake.Kwa namna yoyote ile, chama hicho kinaonekana hakichangamani kimatendo na nembo zinazokipambanua katika bendera yake.

Bendera ya CCM ina nembo ya jembe na nyundo, jembe likiwakilisha wakulima na nyundo wafanyakazi. Rangi ya kijani inabeba bendera ya chama hiki, ikiashiria maisha bora kwa wanachama wake, lakini pia maana hii inazua maswali zaidi sasa ambapo hali ya maisha ya wananchi hasa kundi la wakulima na wafanyakazi inazidi kuwa duni kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

Wakulima wameweka rehani kazi yao kwa wafanyabiashara na serikali, hasa inapokuja suala la bei za mazao na uzalishaji wenyewe. Ukame umekuwa kero na hakuna mkakati wa kilimo cha manufaa, kilimo kinachozingatia umwagiliaji na chenye kutumia zana za kisasa na chenye muelekeo wa kuboresha uzalishaji.

Mfano, zao la korosho linakosa ununuzi na serikali, inaonyesha kushindwa kuwadhibiti wanunuzi ambao ni wafanyabiashara wa zao hilo. Mazao kama pareto, katani, karafuu, pamba na mengine ya biashara hayawanufaishi tena wakulima. Ulimaji wa mazao haya umebakia wa rasharasha na hakuna mikakati ya wazi ya kukuza uzalishaji wake. Bei za mazao hayo zimekuwa zikishuka bila kuwiana na kupanda kwake, huku gharama za uzalishaji zikionyesha wazi kupanda hali inayowafanya wakulima kutoona faida.

Huku ni kushindwa kwa CCM, chama ambacho kimeendelea kunufaika na kutawala dola tangu kuzaliwa kwake, licha ya kuwa Tanzania sasa inafuata mfumo wa vyama vingi, mfumo uliopitishwa na kuanza mwaka 1992. Hali hii ni tofauti na nchi za jirani kama; Malawi, Kenya na Zambia ambazo vyama vyao vyenye umri unaokaribiana au kuzidi ule wa CCM vilishapigwa mweleka katika chaguzi za vyama vingi.Kama kuna mafanikio katika maisha ya watanzania hakuna uwezekano wa kuyatenga na sera za CCM, na kama kuna kudorora kwa maendeleo CCM inahusika pia.

Ukweli kuna kushindwa katika muendelezo wa sera za CCM na chama sasa hakiwezi kusimama na kutangaza itikadi yake na mikakati yake ya muda mrefu kama ilivyokuwa wakati wa uanzishwaji wake mwaka 1977.Wafanyakazi wa Tanzania wako katika hatihati siku zote tangu kuingia sera za ubinafsishaji, sera zilizoambatana na upunguzaji wa wafanyakazi, kupungua kwa ajira katika sekta rasmi na pia kufa kwa viwanda mbalimbali nchini.Eneo pekee ambalo linaonekana kuwa kauli mbiu ya viongozi wa CCM ni biashara, nchi haijaweza kuzalisha soko la ndani kwa ajili ya bidhaa za humu lakini imezidi kuzungumzia suala la ujasiliamali.

Wafanyabiashara wana nguvu ya maamuzi katika chama kufuatia uwezo wao wa kukifanya chama kifanye kazi. Chama hiki licha ya kujirithisha mali zote zilizozalishwa wakati wa mfumo wa chama kimoja, bado hakijaweza kujiendesha na uhakiki wa mali zake unazua maswali.Miradi mbalimbali ya chama hiki ilikufa na baadhi ya mali zake kutumiwa na wajanja wachache.

Chama sasa hakitegemei tena ada ya wanachama wake badala yake michango ya wafanyabiashara na matajiri. Chama sasa kinazungumzia sera za ustawisho kwa matajiri maana ndio wana nafasi pia ya kuchaguliwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Mwana CCM maskini anabaki na nafasi ya kupiga kura tu na hawezi kuchaguliwa.

Chama sasa kinawatumia matajiri katika kuwania nafasi mbalimbali ili kurahisisha wao kutumia nguvu zao kiuchumi kujipigia kampeni na pia kusaidia wagombea wengine wa chama hicho. Inachikifanya sasa CCM ni kusaka viti vingi katika nafasi za uwakilishi na sio kugombania kupata viongozi bora, wenye dira na nia ya kuendeleza nchi na watu wake.Kwa hali hii nafasi ya maamuzi kutoka kwa raia wa chini, wakulima na wafanyakazi ni finyu.

Hali hii inahatarisha maisha ya kundi kubwa la watu ambao ni maskini nchini, kufuatia wawakilishi kutokuwa na mipango ya wazi ya namna ya kuendeleza vipaumbele vya maendeleo katika nchi.

Monday, January 29, 2007

Kamera ya X-ray kuvua watu nguo

Iwapo Kamera hii itatumika kudhibiti ugaidi, kama STORI hii inavyosema, basi tutakuwa kama vile tunatembea uchi.

Kikwete vua ngozi ya Mkapa uwe shujaa


Na Ansbert Ngurumo, Hull

TUNAMPENDA rais wetu, lakini hatupendi baadhi ya tabia zake. Ndiyo maana tunamwambia haya. Ndiyo maana namuuliza maswali. Namwandama? Hapana! Nimuulize nani?

Maana, kama ningekuwa na swali moja tu, nikaulizwa nimtaje mtu mmoja katika Tanzania nzima ambaye, ikibidi awe wa mwisho kufa – kabla yangu – ili aulizwe swali hilo, nimgemtaja rais. Ndiyo! Rais Jakaya Kikwete, chaguo la mtandao, ‘mtu wa watu,’ chaguo la mwisho la Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nimeandika maneno hayo hapo juu makusudi. Kuna waliowahi kumwita ‘chaguo la Mungu.’ Wakaleta hisia za ubaguzi na mgawanyiko miongoni mwa Watanzania. Maswali yakaibuka. ‘Kama huyu ni chaguo la Mungu, wengine ni chaguo la shetani?’ Maneno kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu yalisemwa kwa mara ya kwanza na Padri mmoja pale Manzese, Dar es Salaam; anaitwa Mapunda, ‘Tunda Kanisa.’ Bila shaka aliyasema kwa ushabiki, hakutumwa na Kanisa, maana yeye si msemaji wa Kanisa.

Bahati mbaya, maneno hayo yakasingiziwa kwa maaskofu wa Kanisa Katoliki! Baadaye ilijulikana kuwa kundi kubwa la maaskofu hao, na katika umoja wao bila kusema rasmi, walishatekwa na mtandao wa Kikwete, kwa jina la CCM, kumuunga mkono Kikwete. Leo baada ya mwaka mmoja na ushehe, wanajutia ushabiki wao kwa Kikwete? Ndiye huyu waliyemtarajia? Ni kweli alikuwa chaguo la Mungu au la mtandao?

Nitaeleza kidogo kwa nini nasisitiza chaguo la mtandao! Yaliyotokea ndani ya CCM tunayajua. Chama hakikuwa na chaguo, bali makundi ya wanachama na ya viongozi yalikuwa na ‘machaguo’ yao. Kikwete alikuwa wa mtandao, ambao uliyapiku makundi mengine, na baadaye kumhalalisha Kikwete kwa wana CCM wote.

Ndivyo alivyopata sifa nyingi baadaye. Hata waliokuwa hawamwamini ndani ya chama wakaongoza katika kuimba: “Nina imani na Kikwete, iya , iya, iya…Kikwete kweli….” Pole pole, akawa chaguo la mwisho la CCM. Wakamnadi kama chaguo la watu. Na waliosimamia uchaguzi wakatueleza kwamba ameshinda uchaguzi; akawa rais wetu ‘mwenye mvuto.’

Sina shaka mvuto huo bado anao. Hata juzi alipokuwa hapa nchini Uingereza kwa safari ya kikazi, alishuhudia umati wa Watanzania waliokusanyika kumlaki, kumsalimia, kuteta naye na kumuuliza maswali. Ubalozi wa Tanzania nchini hapa ulifanya maandalizi makubwa ya kuwakusanya Watanzania wengi. Walifika. Pichani kulia, Rais Kikwete akiwa na mkewe na viongozi wengine, anawahutubia Watanzania katika ukumbi wa hoteli ya Churchhill, London.

Waliokuwapo hawajaacha kusimulia badhi ya mambo yaliyojitokeza; kwamba ukumbi uliopangwa haukutosha. Viti viliongezwa. Rais mwenyewe alichelewa kwa dakika zipatazo 45 (kama alivyokuwa akifanya akiwa waziri). Baadhi wanahoji: “kumbe urais haujambadilisha?”

Wanakumbuka hotuba yake ndeeeefu (kuhusu karibu kila kitu alichofikiria kuhusu Tanzania). Wengine wanasema ilikuwa ndefu mno bila sababu. Wanakumbuka nyimbo za CCM zilizoporomoshwa ukumbini, na baadhi ya washiriki ‘waliovalishwa’ sare za chama na kupewa bendera za CCM. Aliyewapa nani? Balozi wa Tanzania nchini Uingereza! Kwani ulikuwa mkutano wa CCM? Wanajua wao.

Kilichowaudhi? Hotuba ndefu iliyomaliza muda wote aliokuwa amepangiwa Rais Kikwete kuzungumza na Watanzania. Badala ya kuzungumza nao, akawahutubia. Hilo liliwaudhi Watanzania waliokuwapo. Hotuba ya dakika 90 ya nini?

Wakosoaji wake wanadai alifanya hivyo ili kukwepa maswali. Na kweli, hakuna Mtanzania aliyeuliza swali. Alipomaliza kuzungumza, akasema muda wake umekwisha, na kwamba wenyeji wake walikuwa wamempangia ratiba nyingine ya kukutana na Waziri anayeshugulika na masuala ya Afrika.

Alijua wana maswali – na ndiyo maana wanasema aliyakwepa. Maana aliwaaambia kuwa wenye maswali wayatunze hadi tarehe 17 Februari 2007 atakaporejea Uingereza kwa ziara nyingine yenye ratiba nafuu. Kikwete huyo! Akaondoka ukumbini, kwenda katika kikao hicho cha kikazi.

Watanzania walisikitika baadaye walipogundua – baada ya muda mfupi – kuwa hakwenda kukutana na waziri huyo, bali alikua katika mechi ya soka kati ya Tottenham Hotspurs na Newcastle. Walisikitika!

Licha ya baadhi ya wapenzi wake, ubalozini na nje ya ubalozi, kutetea kitendo hicho cha rais Kikwete, wakisema asingeacha kwenda kwa kuwa alikuwa amepangiwa na wenyeji wake; wakosoaji wamekuwa wakisema – hadi leo- kwamba wenyeji wa rais hawampangii rais kwenda kwenye starehe ambazo hajaziomba au hajaziafiki.

Wanasema ana haki ya kufurahi kama binadamu wengine, hasa kwa kuwa yeye anajulikana ni mpenzi wa soka. Lakini si soka lililomleta Uingereza. Na alipewa fursa ya kuchagua kati ya kuwa na Watanzania kwa walau dakika nyingine 15 ili wamhoji maswali, yeye alichagua mpira!

Ilisikika baadaye kuwa kesho yake alipata fursa ya kujumuika kwa muda wa kutosha na wana CCM waishio London. Alijua hawa wasingekuwa na maswali muhimu bali nyimbo na tenzi. Maana kwao, yanapofika matendo, CCM kwanza, Tanzania baadaye!

Ikumbukwe kuwa wananchi hao waliokusanyika pale walitoka sehemu mbalimbali za Uingereza. Si wote wanaoishi London. Rais angekwenda uwanjani, lakini angewapa muda wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali. Alikuwa na uwezo wa kutoa hotuba fupi. Aliirefusha kama mkakati wa kuwakimbia. Na baadhi yao bado wanahoji. Alitaka kuficha nini? Au kuna uhusiano na hili sakata la rada? Maana ni wiki hiyo hiyo limezuka akiwa London.

Alipohojiwa na vyombo vya habari vya huku, Rais wetu akaonyesha ushabiki wa ununuzi huo wa rada. Anasema ilikuwa ya lazima. Lugha ile ile ya mawaziri wetu Bungeni! Akazungumzia kukerwa na bei ya rada hiyo. Hakukerwa na ‘dili’ ya ununuzi wake. Hakukerwa na taarifa za rushwa. Walau hakuonyesha kukerwa.

Sasa, baadhi ya hao aliowakimbia London, wanahoji. Rais wetu, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati rada inanunuliwa, alichangiaje katika upatikanaji wa ‘dili’ hiyo? Alipata nini?

Kwa nini asichunguzwe sambamba na rais aliyekuwapo; mwanasheria mkuu wa serikali aliyekuwapo; gavana wa benki kuu; waziri wa fedha; waziri wa mawasiliano na uchukuzi; maofisa wa juu jeshini; na wengine wanaohisiwa kuhusika, ama moja kwa moja au kwa mzunguko?

Maswali haya yanaulizwa miongoni mwa Watanzana huku Uingereza, na kituo kimojawapo cha redio ya kwenye mtandao wa kompyuta kilichopo Marekani kimerusha kipindi kirefu kuhusu sakata hilo.

Sasa kinachojadiliwa pia ni kulindana kunakojitokeza ndani ya serikali yetu. Mnyororo wa uhusiano kati ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa na hii ya nne ya Kikwete, hauwezi kuleta manufaa kwa Wanzania. Unamnyima rais ujasiri wa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa. Anaogopa asichukue hatua ambayo ikichunguzwa, naye atahusishwa kwa kuwa alishiriki katika ngazi fulani.

Mashabiki na wapenzi wa Kikwete wanaona sakata hili la rada linamgusa Mkapa. Wanataka wananchi na dunia nzima imwangalie Mkapa na watu wake. Wanasahau kwamba wakiitwa watu wake, Kikwete atakuwamo. Bado wana imani kwamba Kikwete anaweza kuwachukuliwa hatua wakubwa walioshiriki.

Wanakumbuka, na bado wanaamini kauli zilizokuwa zinasambazwa na wanamtandao, kwamba wanataka kuwaondoa wazee hawa – tena baadhi yao waliwaita “hii mijitu” – ili kujenga Tanzania mpya. Wanaona Kikwete na washirika wake wa sasa wana nguvu za kuchukua hatua nzito na kurejesha heshima ya serikali, na kukinusuru CCM kutoka kwenye shutuma za kuwa Chama Cha Majambazi. Watanzania hawa wanawaamini viongozi wetu wa sasa.

Mimi nasema, “ndiyo tunawaamini, lakini wanaaminika? Wanajiaminisha? Wanaamini kwamba Tanzania yenye neema inawezekana. Nami naamini hivyo, lakini nauliza, “itawezekana chini ya mfumo huu na kwa utaratibu huu?” Baadhi yao wanaamini kwamba Kikwete anaweza kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.

Nami nayataka; nayatamani maisha hayo. Ila sioni kama yanakuja. Sioni maandalizi. Sioni tofauti, bali marudio. Wapo walioamini kauli za wanamtandao, waliojiaminisha kwa Watanzania kwa ‘kumkandia’ Mkapa; na kwamba muarobaini wa matatizo ya Watanzania ni Kikwete. Leo wana jeuri ya kusema hivyo?

Kikwete ninayemuona ni huyu. Ni Mkapa mwingine katika sura tofauti. Na Kwa kuwa alijipatia umaarufu kwa kujitofautisha na akina Mkapa jukwaani, ajue kwamba hawezi kukubalika zaidi na kuaminika kwa Watanzania hadi hapo atakapojitofautisha kwa vitendo. Kikwete wetu amevaa ngozi ya Mkapa. Si aivue tumwone shujaa?

Uchambuzi huu umechapishwa katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili, 28. 01. 2007. Mwandishi anapatikana kwa simu +447828696142 na barua pepe ansbertn@yahoo.com.

Shilpa aliyebaguliwa aibuka mshindi Big Brother UK


Unamjua Shilpa Shetty, mwigizaji maarufu wa Bollywood ya India? Mtazame hapo pichani kushoto. Ndiye mshindi wa mwaka 2007 wa Big Brother, Uingereza. Baada ya masaibu yaliyomkuta, sasa ameibuka kidedea. Soma habari zake HAPA.

Sunday, January 28, 2007

Karume ndiye mwenye ufunguo Zanzibar


Na Ndimara Tegambwage

ZANZIBAR yaweza kuwa chimbuko jingine la “kuchafuka kwa hali ya hewa kisiasa,” ambako kulimfukuzisha urais, Aboud Jumbe.
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa anataka kumaliza kile anachokiita “mpasuko” wa kisiasa katika visiwa ya Unguja na Pemba na kwamba hataki mwanachama yeyote wa chama chake, CCM awe kikwazo.
Hili ni kama apizo. Kwanza Rais Kikwete amesema na kurudia kwamba amedhamiria kumaliza “tatizo la Zanzibar.” Lakini katika apizo anasema hataki mtu yeyote kumchafulia.
Amesema atakayejiingiza na kujaribu kuzuia juhudi za kuleta ufumbuzi, atafukuzwa uanachama wa CCM. Si kawaida kwa rais kutumia vitisho vya aina hiyo katika suala linalohusu utatuzi wa mgogoro.
Kikwete alisema kama rais, lakini amevaa kofia ya mwenyekiti pia wa CCM. Je, inawezekana ni uenyekiti wake unaofanya atishie kumvua mtu uanachama au kuna jambo la nyongeza? Je, wenye nafasi ya kutibua ufumbuzi ni wale wa CCM peke yao?
Je, inawezekana rais au mwenyekiti wa CCM amegundua kuwa mpasuko wa Zanzibar umeletwa na kulelewa na viongozi wa CCM au wanachama wake, na si wananchi kwa ujumla au wanachama na viongozi wa Chama cha Wananchi – CUF? Kwa nini rais atishie kumvua uanachama, mtu au tuseme kiongozi yeyote wa CCM?
Kwa kuzingatia hali ya Zanzibar, ufunguo wa mgogoro ulioghubika nchi hiyo, ni Rais Aman Karume. Kulainika kwake kunaweza kufanya mgogoro uyeyuke na kukamia kwake kunaweza kufanya hata juhudi za Rais Kikwete kukwama.
Mazungumzo yanayoendelea hivi sasa kati ya CCM na CUF, yakiongozwa na makatibu wake wakuu, Yusufu Makamba na Maalim Seif, ni hatua ya kukamilisha kile ambacho Rais Kikwete ameishaandaa.
Bila shaka Kikwete atakuwa ameandaa kwa ushirikiano na Rais Karume. Vinginevyo ameandaa na wahasimu wa Karume ndani ya CCM na huko huko visiwani. Hili linajitokeza katika sura mbili.
Kwanza, ni ukaidi wa CUF kwamba hata sasa hawatambui ushindi wa Karume na hawako tayari kuingia katika muwafaka wa tatu. Hili linaonyesha CUF wanaweza kuwa wameona mzani unaelemea upande upi na wanataka kutumia karata yao kufanikisha majadiliano ya sasa.
Kwani Karume, kama Rais Mstaafu, Salmin Amour, hajatimiza matakwa yote ya muwafaka wa pili kati ya CCM na CUF na huenda akatoka madarakani bila kuutekeleza wote.
Pili, ni jinsi Yusufu Makamba alivyokwenda Zanzibar. Katika mazingira ambayo inasemekana Naibu Katibu Mkuu wake, Salehe Ramadhani Feruzi “alimkimbia,” bila shaka kuna mambo ambayo hayaendi sawa katika mpangilio wa kumaliza mpasuko.
Feruzi, pamoja na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, ni miongoni mwa marafiki wakubwa wa Rais Karume. Kutokuwepo kumlaki Makamba, uwanja wa ndege na ofisini, kunaashiria upinzani, aghalabu wa chinichini, wa kile ambacho Makamba na Kikwete wanajaribu kunadi.
Habari zisizothibitishwa zinasema pamoja na ujumbe wa Makamba kwa viongozi wa CCM Zanzibar na CUF, alibeba pia vitisho vingi kwa Rais Karume, zikiwemo shutuma hapa na pale, ili kumlainisha na kuzuia upinzani kwa hoja za Kikwete.
Hata hivyo, hiyo ni hali iliyotegemewa. Karume hawezi kukubali haraka kufanya kazi na mahasimu wake; lakini hawezi kuasi uamuzi wa chama chake. Yote mawili ni shubiri kooni.
Rais Kikwete anajua yote haya mawili. Anajua hali inayomkabili Karume ikiwa ni pamoja na upinzani mkubwa ndani ya CCM kutoka kwa waliokuwa wakimuunga mkono au walioshindana naye kuwania uteuzi wa kugombea urais mwaka 2005.
Katika hali hii, nani, kama si Rais Karume, ambaye Kikwete alimlenga, pale alipotishia kwamba atakayekuwa kizingiti katika kuleta ufumbuzi atafukuzwa uanachama CCM?
Kwani uanachama wa CCM unawauma sana viongozi na “wakubwa” wengine, ambao huweza kupoteza nafasi zao za uongozi, hata urais wa Karume, kuliko wanachama wa kawaida.
Wachunguzi wa siasa za CCM wanasema kilichompata Jumbe kinaweza kumpata Karume iwapo atakaidi mapendekezo ya Kikwete. Kwanza kwa kutangaza hali ya kuchafuka kwa siasa, ambazo hakika zilichafuka tangu zamani, na pili kutafuta njia ya kumweka kando kupitia Dodoma.
Rais Aman Karume alipigiwa kampeni kubwa Dodoma na Kikwete na wenzake, mwaka 2000 kwa tiketi ya vijana. Vikao vyote vya juu ya CCM vilizizima kwa kampeni za “kijana Zanzibar” na kwamba chaguo pekee alikuwa Aman Karume.
Leo hii, wakati Rais Kikwete anataka kuondoa kile alichoita mpasuko Zanzibar, si tu anahitaji, bali pia analazimika kupata, ushirikiano wa “ndugu yake katika siasa za ujana za 2000.
Lakini iwapo ushirikiano hautapatikana, na iwapo Kikwete na Karume hawatakuwa na msimamo mmoja, uwezekano wa Kikwete kumtosa Karume, tena pale Dodoma, kupitia vikao vya CCM, uko wazi kabisa.
Wachambuzi wa siasa wanauliza iwapo Kikwete anaweza kumtosa Karume ili kumaliza mgogoro, ambao kumalizika kwake kunaweza kuondoa CCM madarakani huko Zanzibar na huenda kuwa njia pekee ya kuimarisha upinzani Tanzania bara.
Kwa kila hali, na hata bila kuanza kwa majadiliano ya kina, mwenye uwezo wa kuleta ufumbuzi wa haraka Zanzibar ni Rais Aman Karume. Huo ndio ufunguo.
Kinyume cha hayo, Kikwete ana uwezo, kupitia Dodoma, kuweka mazingira yatakayozaa shutuma na hata kashfa, na hatimaye kujiuzulu au kufukuzwa kwa Karume katikati ya vilio na aibu. Lakini yote kwa faida ya nani?
Kuchafuka au kutochafuka kwa siasa; kufukuzwa au kujiuzulu kwa Karume; jawabu sahihi kwa mgogoro wa Zanzibar ni kuheshimu kauli ya umma. Kuacha kuchezea maamuzi ya wananchi katika sanduku la kura.
Uadilifu ukitinga, haki ikatendeka, aliyeshinda ataingia ikulu; aliyeshindwa atasubiri wakati wake bila kelele wala mikwaruzo.

ndimara@yahoo.com
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'